Hivi karibuni Diamond
aliamua kuweka ‘ego’ pembeni na kukiri kuwa Jokate Mwegelo ndiye msichana
katika maisha yake aliyemkosea sana na anajuta kumuumiza
Diamond alifunguka
hayo kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV, kilichorushwa wiki iliyopita.
Akiongelea jinsi
alivyomuumiza Jokate, Diamond alisema, “Kwasababu alikuwa too innocent halafu
hakuwahi kunikosea kitu chochote Jokate kabisa, halafu nikamwingiza kwenye
matatizo, watu wakamchukulia tofauti kwamba ‘Jokate kamchukulia Wema boyfriend
wake’ wakati nilimfuata mimi kama mimi, nilimtafuta mwenyewe halafu then nikawa
niko naye halafu ghafla nikarudisha mahusiano kwa Wema. Sikujiskia vizuri
halafu still haikuwa vizuri so sometimes nikikaaga hivi nasema nilimkosea.”
Akijibu swali la
kwanini alimuacha Jokate, Diamond aliongeza, “Sijui nilirogwa hata sijui, I
don’t know, sijui hata kwanini, hakuwahi kunikosea chochote sio, sababu
nilikuwa nikikaa naye alikuwa akinishauri vitu vingi vya maendeleo, sijui
ulikuwa ni utoto sielewi yaani, sijui ni kitu gani, nilijikisa vibaya sana,
halafu mtoto wa watu mstaarabu sana, alijitahidi kujenga career yake sasa hivi
imekaa vizuri.”
Bongo5 imewasiliana na
Jokate ili kutaka kufahamu upande wake baada ya kusikia kauli ya Diamond
aliyesema anafurahi kuona Diamond amefunguka ukweli.
Watu wengi hawajui
the real issue, I’m glad kama ame-acknowledge I was innocent in that whole
matter,” amesema Jokate.
No comments:
Post a Comment