EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, July 31, 2013

CHOMBEZO: KITANDA CHA MAMA MWENYE NYUMBA....SEHEMU YA.... 01

Mtunzi_Na: IRENE MWAMFUPE NDAUKA
 “Mke wangu, kila
siku namwona huyu kijana mchafuchafu anakuja kuokota chupa tupu hapa, ina maana
tuna chupa tupu kila siku?”
“Siyo hivyo mume
wangu, we hujamfuatilia tu, anakuja kila baada ya siku tano. Tumsaidie mume wangu,
si unamwona kijana mwenyewe masikini huyu,” alisema mama Joy huku macho yake
yote yakimwangalia yule kijana mwokota makopo…
 
“Awe anakuja
mchana basi, usiku kama huu hapa nje, mimi naweza kumchapa risasi nikidhani
mwizi. Si unaona hata mavazi yake? Kwanza haogi huyu, hata harufu anatoa…”
 
“Mume wangu
usimkufuru Mungu, sisi kupewa uwezo ni matakwa yake, hakuna binadamu ambaye
akipewa nafasi ya kuchagua maisha bora na duni, atasema anataka duni.”
“Mimi sijafika
huko, ila nasema awe anakuja mchana tu  si usiku kama huu.”
 
“Sawa mume wangu,”
alisema mama. Hayo yalitendeka  wakati
baba Joy akiegesha gari mahali pake kisha akashuka na kuanza kutembea mkononi
ameshika brifkesi yake. Siku hiyo, baba Junior alikuwa kama amevaa Kinaijeria
f’lani.
 
Mama Joy alimpokesa
mumewe brifkesi kisha akamwacha apite ili yeye amfuate kwa nyuma. Wakati mumewe
anaingia, mama Joy aligeuka kumwangalia mwokota chupa tupu ambaye kwa muda huo
alikuwa amebeba fukp la ‘salfeti’ begani.
 
Mama Joy alimwonesgha ishara kwamba aondoke haraka sana kwa vile mumewe amerudi. Kijana
wa watu, alitoka getini kwa kuruhusiwa na mlinzi.

“Unasikia mama
Joy,” baba Joy alianza kusema tena akiwa amekaa kwenye sofa kubwa…
“Abee…”
 
“Mimi sipendi watu
wawe wanaingiaingia humu ndani hovyo. Tena nadhani iko haja ya sehemu ya
kutupia taka niijenge nje ili watu wasipate sababu ya kuingia ndani…
 
“Wewe kijana
mchafuchafu vile, si lazima pia atakuwa mwizi..?”
“Nimekuelewa baba
Joy, hataingia tena usiku ikitokea itakuwa mchana.”
 
“Iwe hivyo, sitaki
kumwona tena usiku. Kwanza wewe ni mke wa mtu, mnachekeanachekea kwa sababu
gani?”
 
“Basi mume wangu
jamani, nimekuelewa.”
Mzee huyo aliondoka kwenda kazini, mkewe
mama Joy alisiama nje kwa muda mrefu, alipotaka kugeuka kurudi ndani, kwa mbali
alimwona mwanaume akitokea. Mgongoni alibeba furushi…
 
“Au yule?” alisema moyoni. Alisubiri kwa
muda ili amwone kwa karibu, lakini hakuwa yeye.
Nusu saa baada ya kuingia ndani, kengele ya
geti kubwa ililia…
 
“Mh! Si yeye huyo?” alijihoji mama Joy
akiamini aliyebonyeza kengele ni mzoa taka. Japokuwa alijua mlinzi
atashughulikia, lakini aliamua kutoka mwenyewe kuelekea getini ambapo alimkuta
mlinzi anasukuma geti kubwa.
 
 “Nani
amepiga kengele?” mama Joy aliuliza…
“Sijamjua ni nani?” mlinzi alijibu huku
akiendelea kusukuma geti, likawa wazi…
“Shikamoo mama,” mzoa taka alisalimia akiwa
anatabasamu...
“Hujambo wewe?”

badala ya kusema marhaba. Na tangu mzoa taka huyo ameanza kuingia ndani ya
nyumba hiyo kuchukua taka, kila akimsalimia shikamoo mama Joy anajibiwa hujambo
wewe au asante kijana…
 
“Sijamboo, shikamoo…”
“Asante…askari, funga geti…”
“Sawa. Huyu mzoa taka aingie..?”
 
“Aingie ndiyo. Akishaingia funga geti.”
Mzoa taka aliingia hadi ndani, akamkaribia
mama Joy ambaye naye alimkaribisha hadi kwenye sehemu yenye taka.
Mlinzi aliwakodolea macho. Kilichomshangaza
zaidi ni kauli ya baba Joy kwamba hataki kumwona mlinzi huyo nyumbani kwake…
 
“Sasa mbona amemuingiza tena leo? Halafu
kuna siri nzito mimi naiona kati ya mama na huyu mzoa taka, maana mama
akiamkiwa shikamoo hatakagi kuitika marhaba,” mlinzi aliwaza.
 
Mama Joy alimfikisha mzoa taka kwenye pipa
la taka ambalo lilijengwa vizuri ndani ya nyumba hiyo…
“Jana mwenzangu mzee alikasirika sana,”
alianza kusema mama Joy…
 
“Hata mimi kama nilimwona. Niliogopa sana…”
“Yeye anasema hataki kuona unaingia humu
ndani usiku. 

Akasema atalitoa hili pipa na kulijengea nje huko.”
“Kwa hiyo akinikuta saa hizi humu ndani
kwake si ataniua?”
 
“Hawezi, ingawa ana bastola…”
“Mama mimi nakwenda, kumbe mumeo ana
bastola..!”
“Hawezi kukuua, alisema hataki uingie usiku,
‘asa kwani saa hizi ni usiku?”  

JE NINI KITAENDELEA ...USIKOSE...SEHEMU YA ....02... 
Kuwa na mimi hapa tena siku ya Jumamosi itaendelea.....

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate