Mwigizaji wa filamu za Kibongo,
Irene Pancras Uwoya, amelowa mvua ya matusi baada ya kumfananisha
mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na aliyekuwa mwanamuziki
mkubwa duniani, marehemu Michael Jackson.
Wikiendi iliyopita, Uwoya aliandika
kwenye ukurasa wake katika mtandao wa Instagram kuwa msanii huyo
anayefanya vizuri katika Bongo Fleva ndiye staa atakayemrithi mkali huyo
wa Pop, maandishi ambayo yalizua matusi hayo ya nguoni.
Baadhi ya mashabiki wa mastaa hao
walitoa maoni kuwa jambo hilo ni sawa na kufananisha vitu ambavyo havina
uwiano hasa ukizingatia Michael Jackson alishafariki dunia Juni 25,
2009.
“Sasa hiyo ni akili gani ya ki…(tusi)
kumfananisha mtu aliyeko hai na marehemu?” alihoji Mishish, mmoja wa
mashabiki wa Uwoya katika mtandao wa Facebook baada ya ishu hiyo kuwa
gumzo mitandaoni.
“Kweli wewe Irene (Uwoya) ni …(tusi)
au kwa sababu Diamond amesha…(tusi) ndiyo maana unamsifia kiasi hicho,”
aliandika shabiki mwingine kwenye Twitter na kupisha wengine kuendelea
kumporomoshea Uwoya matusi ya nguoni
No comments:
Post a Comment