MSANII wa filamu za Bongo, Miriam Jolwa ‘Kabula’ ameonesha kukerwa na
wanaume ambao hawana hela ‘wanaume suruali’ lakini wamekuwa
wakijifanya wanajua kupenda sana huku wakiwa na wivu kupitiliza.
Akipiga stori na paparazi wetu juzikati, Kabula alisema anajua
kupenda ni suala la msingi lakini anawashangaa wale wanaokuwa na wivu wa
kupindukia na wakati mwingine kutoa vipigo kwa wapenzi wao wakati wao
ni wanaume ‘suruali’.
“Unajua nawashangaa sana wanaume wa aina hiyo,
wanakuwa na wivu kupitiliza lakini hawawasaidii chochote wapenzi wao
zaidi ya kuonesha wana wivu kweli na wakipishana kidogo tu kipigo
kinatembea, mimi wananikera sana,” alisema Kabula.
No comments:
Post a Comment