EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, July 31, 2013

KODI YA SIMU KURUDI BUNGENI AGOSTI,NI BAADA YA KUTOKEA UTATA KUHUSU KODI HIYO.

http://www.habarileo.co.tz/images/resized/images/mgimwazz_255_300.jpg

SAKATA la kodi ya simu ya Sh 1,000 kwa kila laini ya simu kwa mwezi, inayolipwa na watumiaji wa simu, litamalizwa bungeni kisheria. Waziri wa Fedha, William Mgimwa, amesema wameanza kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete, la kuitaka Wizara ya Fedha kukutana na wadau wengine, kuangalia namna ya kupata vyanzo vingine vya mapato mbadala wa kodi hiyo.
Alisema hayo alipozungumza jana na gazeti hili, baada ya kusaini mkataba wa msaada wa zaidi ya Sh bilioni 344, kutoka Benki ya Dunia, ili isaidie masuala mbalimbali katika sekta ya usafirishaji. Mgimwa alisema katika suala hilo, masuala ya kisheria yatafikishwa bungeni mwezi ujao, ili kumaliza utata wa kodi hiyo.
 
Alisema uamuzi wa kushughulikia suala hilo, ulifikiwa kutokana na agizo la Rais Kikwete la hivi karibuni, kutaka wizara hiyo na ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kukaa na kampuni za simu kumaliza utata uliojitokeza kuhusu kodi hiyo.
Awali Umoja wa Wamiliki wa Kampuni za Simu (MOAT), ulitoa maoni kutaka kufutwa kwa kodi hiyo, kutokana na kulalamikiwa na wadau wa sekta ya mawasiliano.
Mbali na Moat, pia baadhi ya viongozi wa Serikali, wabunge na wananchi, walipinga kodi hiyo kwa walichokieleza kuwa itaongeza mzigo wa ugumu wa maisha kwa mtumiaji, hususan wa kipato cha chini.Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, alipozungumza na gazeti hili jana, alisema mara baada ya Rais kutoa agizo, wizara husika zilikutana kufanyia kazi agizo hilo.
"Rais akishaagiza kinachofuata ni utekelezaji na sisi kesho yake tulianza vikao na ninachoweza kukwambia tuko pazuri na tukikamilisha majadiliano yetu, tutatoa taarifa," alisema Makamba.
Alisema lengo ni kuangalia kama Serikali inaweza kupata Sh bilioni 178 kutoka vyanzo vingine, iwapo itaamua kufuta kodi inayotokana na tozo ya Sh 1,000 kutoka kwenye laini za simu.
Hivi karibuni, Rais Kikwete aliagiza Wizara za Serikali zinahusika na kodi na mawasiliano na kampuni za simu za mikononi nchini, kukutana kutafuta jinsi ya kumaliza mvutano wa kodi hiyo.
Alitoa maelekezo hayo baada ya kukutana na viongozi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wawakilishi wa kampuni za simu za TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel. Rais alisema lengo kuu la mkutano huo, liwe kupendekeza jinsi ya kuziba pengo la Sh bilioni 178 ambazo zitapotea katika bajeti, iwapo kodi hiyo itafutwa na Serikali kupitia marekebisho kwenye Muswada wa Fedha wa Bajeti ya Mwaka 2013/14.
Aliwaambia wawakilishi wa pande hizo mbili kuwa hawezi kuifuta moja kwa moja kodi hiyo, bila kutafuta njia nyingine za kupata fedha za kujaza pengo litakalotokeza, huku tayari Bunge limezipangia matumizi.
“Nakuombeni kaeni pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili yenu pamoja tutafute namna gani tutajaza pengo hili la Sh bilioni 178, endapo tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha wananchi mzigo mzito na kuwa pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu,” alisema Rais Kikwete.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate