JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro limewaua kwa kuwapiga risasi watu wawili wanaodhaniwa ni majambazi.
Pia, linawashikilia wengine watatu, wanaotuhumiwa kushiriki katika matukio mbalimbali ya uhalifu katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
Pamoja na watu hao, jeshi hilo linamshikilia mtoto mdogo wa kiume mwenye umri wa miaka tisa (jina lake limehifadhiwa), ambaye hutumiwa na majambazi kufungua milango na kupenya maeneo yenye nafasi ndogo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Robert Boaz, alisema tukio hilo lilitokea Julai 2 katika msitu wa Njoro Manispaa ya Moshi baada ya watuhumiwa hao kutaka kutoroka chini ya ulinzi wa polisi.
Alitaja waliouawa ni Adriano Mkwizu (38), mkazi wa Unga Limited Arusha na Wilhelm Millian (35), mkazi wa Maeda Mwika mkoani Kilimanjaro, ambao awali walikamatwa baada ya kutajwa na wenzao, kuhusika katika matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha.
Kamanda alisema kabla ya kuuawa watu hao, wote kwa pamoja na wengine ambao majina yao yamehifadhiwa, walikamatwa eneo la Unga Limited jijini Arusha Julai 2 na kuhojiwa, ambapo walikiri kushiriki matukio ya ujambazi.
“Baada ya kukiri walikubali kwenda kutuonyesha sehemu wanazoficha silaha zao… waliwapeleka polisi eneo la Njoro kuonyesha silaha walizoficha, huko ndipo walipotaka kutoroka chini ya ulinzi,” alisema.

Alisema wakiwa eneo la tukio (Njoro), watuhumiwa hao wakionesha eneo walikoficha silaha zao, ghafla waliamua kukimbia. Polisi walipiga risasi hewani kuwataka wasimame, lakini hawakusimama, ndipo walipopigwa risasi na kusababisha vifo vyao.
Boaz alisema baada ya kuuawa watu hao, msako ulifanyika eneo la tukio Julai 3 na kufanikiwa kupata risasi mbili za bunduki aina ya shortgun, risasi mbili za bastola na bastola bandia.
“Baada ya uchunguzi kufanyika nyumbani kwa mtuhumiwa Mkwizu, polisi ilikuta vifaa vya kuvunjia milango, mapanga, mafuta ya kusafishia bunduki vikiwa vimechimbiwa ardhini na televisheni tatu, deki mbili, mapanga matatu, kufuli, funguo…”alisema.
No comments:
Post a Comment