EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, August 31, 2013

CHOMBEZO: KITANDA CHA MAMA MWENYE NYUMBA....SEHEMU YA 06.

Na Irene Mwamfupe Ndauka.
ILIPOISHIA...
 “Haa! Mume wangu huyo anapiga…
“Haloo…”
“Uko wapi wewe..?”
“Nani mimi..?”
“Unaniuiliza swali gani hilo..?”
“Niko nyumbani…”
“Na nani..?”
“Nani mimi..?”

“Mama Joy…”
“Abee…”
Baba Joy alikata simu. Alianza kuhisi kitu
kikubwa zaidi. Akampigia mfanyakazi wa ndani…
“Za safari bosi..?”
“Njema, upo nyumbani..?”
“Ndiyo bosi…”
“Mama je..?”
“Yupo bosi…”
“Yupo na nani..?”
 
“Nani mama..?”
“Hivi nyiye hapo nyumbani pana nini leo..?”
“Kwa nini bosi..?”
“Mbona hammalizi kujibu badala yake mnauliza
maswali… nimekuuliza mama je, yupo hapo nyumbani? Badala ya kunijibu unaniuliza
na wewe ‘nani mama?’” alifoka baba Joy…
“Samahani sana bosi, mama yupo na mgeni
wake…”
 
“Mgeni gani…?”
“Kijana mmoja hivi…”
“Huyo kijana we unamjua..?”
“Namjua bosi, anakujaga kuzoa taka...”
“Kumbe ni yule mzoa taka siyo?” aliuliza
baba Joy huku akisimama kwenda kuongelea pembeni maana aliona pale siri zake
zitakuwa nje…
“Ndiyo bosi…”
“Wako wapi muda huu..?”
“Naona wapo…ooooo, wapo sebuleni bosi…”

“Yaani huyo mzoa taka anakaa sebuleni kwangu..!”
Moyoni mfanyakazi huyo alisema…
“Ungejua wako chumbani kabisa, ungepaa na
ndege utue Dar ufumanie.”
“Haya, asante sana,” baba Joy akakata simu.
Alisimama kwa muda, kisha akampigia tena mfanyakazi huyo…
“Haloo bosi…”
“Sasa sikia, akiwa anatoka huyo mbuzi
nibip…”
“Sawa bosi.”
Baada ya kukata simu, mfanyakazi huyo wa
ndani alimwangalia mlinzi…
“Unajua bosi amejua..?”
“Hata mimi kaniuliza hivyohivyo. Nilishikwa
na kigugumizi kama wewe mwanzo,” alisema mlinzi…
 
Mzoa taka na mama Joy walitumia dakika kama
ishirini kule chumbani. Wakati wanatoka, mama Joy alitangulia mbele akifuatiwa
na mzoa taka kwa nyuma.
Walizunguka kwenda kwenye dude la taka, mzoa
taka akachukua fuko lake akasindikizwa hadi getini. Alichopewa na mwanamke huyo
anakijua mwenyewe.
Mfanyakazi wa ndani alipogundua hilo alimbip
baba Joy, naye akapiga haraka...
 
“Bosi wametoka tayari,” mfanyakazi alisema
kwa sauti ya chini sana…
“Mama Joy kamsindikiza mpaka wapi?” baba Joy
aliuliza huku akiinua mkono wa kushoto juu na kuutingisha ili aweze kusoma saa…
“Kamfikisha getini tu…”
 
“Haya, sasa sikia, mimi nitarudi kesho,
nikifika mjini sitakuja nyumbani mpaka huyo mwanaharamu aje, kwani si anakujaga
kila siku?”
“Ndiyo bosi.”
“Haya, nashukuru sana ee..?”
“Sawa bosi.”
Baada ya kukata simu, mama Joy alitokea
jikoni…
“We mbona unaongea kwenye simu kwa
kunong’ona sana, unaongea na nani?”

“Shangazi yangu anasema anaumwa sana bosi…”
“Sasa kama shangazi yako anaumwa ndiyo
uongee kwa kunong’ona..?”
“Anasema hajisikii vizuri bosi…”
“Khaa! Sasa asipojisikia vizuri yeye ndiyo
inakufanya wewe uongee kwa kunong’ona..?”
“Nisamehe mama…”
 
“Hapa nyumbani kwangu karibu nitawaachisha
kazi watu maana nahisi kama mmeanza kunifanyia ushushushu kwenye nyumba yangu,
mimi sitaki,” alisema mama Joy akiwa amesimama huku amemshikia kiuno.
Akaendelea…
“Unanichimba siyo?”
“Sikuchimbi bosi…”
“Ulikuwa unaongea na nani? Maana najua siyo
shangazi yako…”
 
“Shngazi bosi, kweli tena…”
“Nikikwambia unipe simu nione nitakuta namba
ya shangazi yako..?”
“Ngoja mama nikwambie ukweli…”
“Niambie…”
“Kuna mzee mmoja wa nyumba ya tatu hapo,
huwa ananitaka. Ndiye amekuwa akinipigia simu kila mara. Sasa hivi amenipigia
anasema kama sina kazi niende tukale japo denda, sasa nilikuwa namuuliza denda
ni nini..?”
 
“Sasa ulikuwa unanificha nini..?”
“Nilijua utakasirika bosi…”
“Nikasirikie nini?”
“Utajua kumbe naachaga kazi nakwenda
kukutana na wanaume nje.”
“Sasa mi nikasirike nini? Wewe si mtu mzima
bwana! Lazima utataka kuguswaguswa, kutekenywatekenywa, kushikwashikwa na
kupewa jotojoto,” alisema mama Joy huku akionesha kwa viitendo maneno aliyokuwa
akiyasema, mfanyakazi huyo akawa anacheka na nguvu ikaanza kumrudia kwa mbali…
 
“Au siyo, mimi sina wasiwasi hata nikikuona
unaingiza mwanaume ndani, ilimradi baba Joy asijue tu, mimi mzungu bwana,” mama
Joy alikazia huku akitoka.
Baada tu ya kuondoka, mfanyakazi huyo
alifuta ile namba ya baba Joy kisha akaminya namba za shangazi yake kama
alitaka kupiga lakini hakupiga.

***
Mzoa taka alikuwa kijiweni na wachafau
wenzake. Mazungmzo yao yalitawaliwa na maneno ya kihuni huku wakichimbana
mikwara kibao…
“Jamani masela ee…kuna mke wa mnene mmoja
ameiva kwangu ileile…kila siku nikienda kuchukua taka ananipa chombo natumia,
ameshaniingia hadi room, yaani yuko sawa ile mbaya.”
 
Wenzake walimkatalia, yeye akawaapia. Alitumbukiza
mkono mfukoni na kutoa elfu hamsini…
“Hii amekata leo baada ya kumwendesha
kitandani, mwanamke hasikii, sura yangu inamponesha kichefuchefu.”
Masela wenzake walianza kumsakama walitaka
aigawe ile elfu hamsini…
“Mwana mzuka basi, ichanechane hiyo fifte,
watu tukaning’nie kwenye sembe.”

***
Mama Joy alitembea hadi kwa mlinzi…
“Hebu fungua geti…”
 
“Unataka kwenda wapi bosi..?”
“Si juu yako kujua..?”
“Mzee anaweza kuniuliza…”
“Kwani hana simu yangu..?”
“Mbona leo alinipigia mimi…”
“Kuhusu nini..?”
“Aliniuliza kama upo.”
Mama Joy alisimama, akageuza…
“Alikuuliza kama mimi nipo? Ukamjibuje..?”
“Nilimwambia upo, akauliza upo na nani..?
sikumjibu…”
 
“Mh!” aliguna mama Joy, akakumbuka muda ule
mumewe alipompigia simu wakati yeye anambembeleza mzoa taka na maongezi yao
yakawa hivi…
Anamwambia
mzoa taka…
 “Haa! Mume wangu huyo anapiga…Haloo…”
“Uko
wapi wewe..?”
“Nani
mimi..?”
“Unaniuliza
swali gani hilo..?”
 
“Niko
nyumbani…”
“Na
nani..?”
“Nani
mimi..?”
“Mama
Joy…”
“Abee…”
Baba
Joy anakata simu.
Mama Joy alianza kuhisi kuna kitu mumewe
amekinasa, akahisi kizunguzungu kichwani…
“Fuko hebu sema ukweli wako, hujamwambia
nipo na mtu mwingine ndani..?”
“Sikumwambia mama, labda kama aliongea na
Helena.” Helena ni yule msaidizi wa kazi za ndani…
 
“Mh!” aliguna mama Joy, akakumbuka mambo
haya…
“We
mbona unaongea kwenye simu kwa kunong’ona sana, unaongea na nani?”
“Shangazi
yangu anasema anaumwa sana bosi…”
“Sasa
kama shangazi yako anaumwa ndiyo uongee kwa kunong’ona..?”
“Anasema
hajisikii vizuri bosi…”
 
“Khaa!
Sasa asipojisikia vizuri yeye ndiyo inakufanya wewe uongee kwa kunong’ona..?”
“Nisamehe
mama…”
Mama Joy aligeuza, akarudi ndani.
Alipitiliza hadi jikoni…
“We dada…”
“Abee bosi…”
 
“Baba Joy alikupigia simu leo..?”
Mfanyakazi huyo kwanza alisita kujibu, akili
ilijipeleleza ili kutafuta je ajibu ni kweli au akatae?
“Hapana bosi…”
“Hebu lete simu yako.”
Helena aliitoa simu haraka sana huku
akionesha unyenyekevu wote. Mama Joy alikwenda kwenye namba zilizopigwa,
hakuiona ya mumewe, akaenda zilizopiga pia hakuiona, ila aliikuta ile ya
shangazi ikiwa ameseviwa kwa jina la ‘Anti Suzy’…
 
“Oke, nisamehe sana kwa kukagua simu yako,
maana kuna mtu ameniambia baba Joy alikupigia…
“Hapana mama, hajanipigia.”
Mama Joy alirudi sebuleni, akakaa kwenye
kochi. Aliwaza kidogo, akampigia simu mumewe.
Sauti ya baba Joy ilikuwa nzito kupindukia…
“Haloo…”
“Halo, baba Joy…”
“Nini?”
 
“Khaa! Asa mbona unapokea simu unaniuliza
nini..?”
“Ulitaka nikuulizeje..?”
“Unajua nataka kukwambia nini..?”
“Wewe mwanamke wewe, usiniletee usanii mimi,
we endelea tu,” baba Joy alikata simu.
Mama Joy alibaki ameishika simu yake huku
mikono ikitetemeka na wasiwasi juu…
“Helena,” kwa mara ya kwanza alimuita kwa
jina mfanyakazi wake huyo…

Tukutane siku ya Jumatano sehemu ya 07....Na IRENE MWAMFUPE NDAUKA.

1 comment:

  1. good story... naitwa JACK nipo Dodoma. Nina simulizi nzuri (love stories) namwomba Irene Mwamfupe tuwasiliane kupitia email... jassonj2012@yahoo.com

    ReplyDelete

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate