Skendo ya mastaa mbalimbali Bongo kutajwa katika biashara na
usafirishaji wa madawa ya kulevya ‘unga’ linazidi kuchukua sura mpya
ambapo tayari majina ya wasanii wawili wakubwa, Wema Isaac Sepetu na
Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ yametajwa huku kinachowaponza
kikijulikana.
Habari zinadai kuwa mastaa hao wameanza
kujutia tambo zao za kutangaza utajiri walionao hivyo kuibua maswali
kuwa huenda wana uhusiano na wafanyabiashara wa dawa za kulevya
ikiaminika ndiyo njia ya haraka ya utajiri.
WEMA
Inadaiwa kuwa kitendo cha Wema kutangaza kununua nyumba, magari ya kifahari na kutapanya fedha ndiko kulikomponza na sasa anatajwa na wengi vinywani mwao juu ya kuhusika katika biashara hiyo haramu.
Kuna madai kuwa bosi huyo wa Endless Fame Productions amehojiwa juu ya suala hilo lakini meneja wake, Martin Kadinda alikanusha uvumi huo.

DIAMOND
Wiki iliyopita, Diamond aligeuka gumzo baada ya kuripotiwa akihusishwa na biashara hiyo huku ikidaiwa kuwa kinachomponza ni utajiri alioupata ghafla.
Wiki iliyopita, Diamond aligeuka gumzo baada ya kuripotiwa akihusishwa na biashara hiyo huku ikidaiwa kuwa kinachomponza ni utajiri alioupata ghafla.
Ilidaiwa kuwa kitendo cha kutangaza kununua
nyumba takriban tano jijini Dar, kumiliki kiasi cha Sh. bilioni moja
kwenye akaunti na kuendesha magari ya kifahari ndivyo vilivyochangia
watu kugeuzia antena za runinga zao kwake kutaka kujua ni matunda ya
muziki tu au kuna kingine.
Madai ya jina la Diamond kutajwa katika
saga hilo yalikwenda mbele zaidi ikielezwa kuwa kitendo cha kusafiri
mara nyingi nje ya nchi huku akipiga picha na watu wanaosemekana
kujihusisha na biashara hiyo nacho kilimponza.
Kwa upande wake,
Diamond alisema kuwa hakuna mtu asiyejua namna anavyotafuta fedha kwa
jasho juani hivyo watu wakimuona akila kivulini lazima wakumbuke kuwa
amechumia juani na hajui chochote juu ya dawa hizo.
CREDIT GLP
No comments:
Post a Comment