MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari
Marangu inayomilikiwa na kanisa Katoliki jimbo la Moshi, (jina
limehifadhiwa) alitekwa na kukufungiwa kwenye hoteli moja ya kitalii
mjini hapa na kufanyiwa vitendo vya ngono kwa muda wa siku nne
mfululizo.
Mwanafunzi huyo anadaiwa kutekwa Agosti 6 mwaka huu na kijana mmoja
(jina linahifadhiwa) mfanyakazi wa kampuni ya simu za mikononi (Airtel)
mjini Dodoma.
Akizungumza jana na Tanzania Daima Jumatano, kaka wa mwanafunzi huyo,
Joseph Temba, alidai mdogo wake alitekwa na mtu huyo na tayari
mtuhumiwa ameshakamatwa.
Alisema walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo Agosti 10, mwaka huu,
katika baa moja akiwa na mdogo wake baada ya raia wema kutoa taarifa za
kuonekana kwake.
Kwa mujibu wa kaka wa mwanfunzi huyo siku ya tukio alipokea simu
kutoka kwa mwangalizi wa wanafunzi (matroni) akimjulisha kutokuwapo
bwenini kwa mdogo wake na ndipo walipoanza kufuatilia na kutoa taarifa
kituo kikuu cha polisi mjini Moshi na kupewa namba Mos/RB/9196/2013.
Alisema siku iliyofuata ya Agosti saba jioni walipokea simu kutoka kwa
watu wa karibu wakiwataarifu kuwapo katika hoteli hiyo mdogo wake
lakini baada ya kufika walinyimwa kuona kitabu cha wageni ili kuangalia
orodha ya majina ya wageni waliofikia hapo ili kujiridhisha kama
mtuhumiwa huyo alikuwapo mahali hapo.
Hata hivyo alisema jioni ya Agosti 10 walipokea taarifa za kuonekana
kwenye baa hiyo mtuhumiwa akiwa na mdogo wake na kuwajulisha polisi na
hatimaye kufanikiwa kumtia mbaroni ambapo hadi sasa bado anahojiwa na
jeshi la polisi.
Chanzo cha kutekwa kwa mwanafunzi huyo ni mawasiliano ya simu baina ya
mtekaji na mwanafunzi huyo ambapo inadaiwa mtuhumiwa huyo alimrubuni
mwafunzi huyo kuacha masomo na kwamba angemtafutia nafasi kwenye
shule kubwa za kimataifa.
Inadaiwa kwamba mwanfunzi huyo alikubaliana na propaganda hiyo na
kutoka shuleni jioni ya Agosti 6 na kumfuata mtuhumiwa kwenye gari lake
na kwenda naye hadi Moshi mjini umbali wa kilomteta 50 kutoka shule ya
sekondari Marangu.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, alisema hana
taarifa za kutekwa kwa mwanafunzi huyo kwa kile alichodai alikuwa
ametingwa na majukumu ya kikazi mjini Arusha na kuahidi kulifuatilia
baadaye.
No comments:
Post a Comment