KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), leo
inatarajiwa kutangaza rasmi mchakato wa uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo
unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, Mwenyekiti wa
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho hilo, Hamidu Mbwezeleni, leo
atazungumza na waandishi wa habari kuelezea mchakato utakavyokuwa,
ikiwamo tarehe mpya ya uchaguzi huo.
“Uchaguzi huo awali ulikuwa ufanyike Septemba 29, lakini kutokana na
sheria mpya za uchaguzi zinazotaka kuwe na siku 60 toka tangazo la
kuanza kwa mchakato, basi kamati itatangaza tarehe mpya ili kukidhi
matakwa ya sheria hiyo mpya,” alisema Wambura.
Alisema Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilikutana Agosti 11 na kisha kikao
kingine Agosti 12, ambapo pamoja na mambo mengine ilijadili maandalizi
ya uchaguzi huo.
Mbali ya Mbwezeleni, Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Moses Karuwa
(Makamu Mwenyekiti), Mohamed Sinani, Chabanga Dyamwale na Kitwana
Manara.
Wakati huohuo, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, chini ya
mwenyekiti wake, Alex Mgongolwa, jana ilianza mchakato kupitia usajili
wa wachezaji wenye matatizo, kikao kinachotarajiwa kuhitimishwa leo na
kutangazwa matokeo.
No comments:
Post a Comment