MAUAJI ya mfanyabiashara bilionea wa Mererani
na jijini Arusha, Erasto Msuya aliyeuawa kwa kumiminiwa zaidi ya risasi 20 kwa
bunduki ya Sub Machine Gun (SMG) yameibua mazito ikielezwa kuwa jamaa huyo
ameacha utajiri wa kutisha.
MAUAJI ya mfanyabiashara
bilionea wa Mererani na jijini Arusha, Erasto Msuya aliyeuawa kwa
kumiminiwa zaidi ya risasi 20 kwa bunduki ya Sub Machine Gun (SMG)
yameibua mazito ikielezwa kuwa jamaa huyo ameacha utajiri wa kutisha.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Erasto
ameacha vitega uchumi vingi ikielezwa kuwa ni miongoni mwa wafanyabiashara wa
Mererani wanaoongoza kwa utajiri mkoani hapa, Kilimanjaro na Manyara.
Erasto ambaye aliuawa na watu
wasiojulikana Jumatano iliyopita saa 7:00 mchana wilayani Hai, Kilimanjaro
akitokea Mererani ni mnunuzi na mmiliki wa machimbo ya madini aina ya tanzanite
hivyo alikuwa ni mtu mwenye fedha nyingi.Na Global Publisher
Hoteli
ya Mezza Luna ambayo ni mali ya marehemu Erasto.
UTAJIRI.
Imefahamika
kuwa katika kipindi cha uhai wake, utajiri wa Erasto ulitokana na uchimbaji na
biashara ya madini ya tanzanite katika mji huo mdogo.
Kutokana na
biashara zake hizo, alimudu kumiliki mali nyingi zikiwemo nyumba za kifahari za
kupangisha na kuishi jijini hapa, Manyara na Kilimanjaro.
ALIISHI KAMA
PEPONI
Erasto
ameacha jumba la kifahari alilokuwa akiishi kama yupo peponi lililopo maeneo ya
Ngaramtoni jijini hapa.
Ilielezwa
kuwa jamaa huyo alikuwa akimiliki maghorofa kadhaa mkoani Arusha na huko
Mererani.
Kwa mfano,
kwa Mererani ndiye mtu wa kwanza kumiliki ghorofa lililopo jirani na stendi
kuu.
MAHOTELI
Habari
zilizidi kumwagika kuwa Erasto ameacha hoteli nyingi, zikiwemo SG Resort na
Mezza Luna zilizopo jijini hapa.
Ilifahamika
kuwa hoteli ya SG aliijenga kwa mabilioni kutoka mfukoni mwake na si mkopo wa
benki kama wanavyofanya matajiri wengine.
NDEGE
BINAFSI
Kama
ilivyokuwa kwa matajiri wengine waliofariki miezi kadhaa iliyopita kama Babu
Sambeke na Wakili Mawalla, Erasto naye alikuwa akimiliki ndege (private jet)
aliyokuwa akiitumia katika biashara zake.
MAGARI YA
KIFAHARI
Pamoja na hoteli
na majumba ya kifahari, marehemu huyo ameacha magari kibao ya kisasa likiwemo
Range Rover Vogue New Model alilokuwa nalo wakati anauawa.
Kwa mujibu
wa mmoja wa wafanyakazi wake (jina tunalo), gari hilo alilinunua hivi karibuni
kwa dola za Kimarekani 250,000 (zaidi ya shilingi milioni 400 za Kitanzania).
Alisema gari
hilo ni toleo la mwaka huu na aliliagiza moja kwa moja kutoka nchini Marekani.
Mbali na
gari hilo, mfanyakazi huyo alieleza kuwa Erasto ameacha magari mengine ya
kifahari kama Mercedes Benz, Range Rover Sport, Toyota Land Cruiser V8 na
magari ya kawaida.
Pia ameacha
utitiri wa magari ya kutembeza watalii kwenye mbuga mbalimbali za wanyama.
VITEGA
UCHUMI
Uchunguzi wa
gazeti hili umebaini kuwa Erasto alikuwa akimiliki makampuni kadhaa ya utalii,
nyumba za kulala wageni ‘gesti’ hasa katika Mkoa wa Manyara.
Kufuatia
kifo hicho, watu waliofurika eneo la tukio walikuwa wakielezea utajiri huo huku
wakizililia mali hizo kwa kuwa ameondoka na kuziacha.
MAZISHI
Habari
ambazo zililifikia gazeti hili dakika za mwisho, zilieleza kuwa mazishi ya
bilionea huyo yalitarajiwa kufanyika leo baada ya makubaliano ya wapi pa
kuzikia kama ni Arusha au Upareni.
NINI
KIMETOKEA?
Erasto
aliuawa na watu wasiojulikana kati ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro (Kia) na Mji wa Bomang’ombe katika Mtaa wa Wasomali eneo la
Mjohoroni wilayani Hai, Kilimanjaro huku ikidaiwa kuwa tukio hilo lilitokana na
visasi hivyo kuzua maswali mengi kuliko majibu.
No comments:
Post a Comment