Jumapili iliyopita katika ukumbi wa bilicanas mwanadada, Aunty
Ezekiel alipigwa chupa na kujeruhiwa vibaya na mwanadada aliyetambuliwa
kwa jina la Ivony Bigirwa katika show ya muziki ambapo wasanii wa muziki
wa kizazi kipya waliopo chini ya kampuni ya Wema Sepetu ya Endless
fame walikuwa wakitambulisha nyimbo zao mpya
Chanzo nini?
Baada ya kufuatilia kwa karibu na kuichunguza habari hii
bongomovies tumegundua kuwa chanzo kilikuwa ni ‘beef’ la kugombania
mwanaume ambaye anasadikika ni mume wa mtu kati ya mwanadada huyo
(Ivony) na Aunty Ezekiel
Ilikuaje?
Mpashaji wa habari hii anasema kuwa wanadada hao walikuwa
ukumbini hapo na ghafla mwanaume huyo aliyetambuliwa kwa jina moja la
Sunday alitokea ukumbini hapo na ndipo patashika hilo likazuka kila
mmoja akidai kuwa jamaa huyo ni wa kwake.
Baada ya vuta nikuvute ndipo uzalendo ukamshinda mwanadada ivony
na kuanza kuzichapa na Aunty kabla ya kuamua kuchukua chupa na kumpiga
nayo na kumjeruhi maeneo ya mkononi
Hali ya Aunty Ezekiel
Kwa sasa hali yam dada huyu iko vizuri na mpaka tunavyoripoti
sasa, habari zinasema amesharuhusiwa kutoka hospitalini kwenda kupumzika
nyumbani.Credit BongoMovies.
No comments:
Post a Comment