BINTI wa miaka 14, Mwanarahab Wamukoya wa Bungoma nchini Kenya jana usiku alijifungua mapacha watatu.
Kwa sasa binti huyo na wanaye hao wa kiume wapo hospitali na hali zao ni nzuri.
Mwanarahab aliwashagaza wafanyakazi wa hospitali ya wilaya Bungoma
siyo kwa kujifunga mapacha watatu bali umri mdogo wa miaka 14 alionao.
Mama wa mapacha hao watatu anaeleza kuwa yeye pamoja na baba watoto
wake mwenye umri wa miaka 16 walitaka kuoana baada ya kupata ujauzito
huo lakini mpango wao haukufanikiwa.
Madaktari katika hospitali hiyo wamefurahi kwa kitendo
alichokionyesha Mwanarahab kwenda kujifungua hospitali na hakufanya kama
mabinti wengi wanaopenda kujifungulia nyumbani.
CREDIT: KTN
No comments:
Post a Comment