Chanzo
cha moto huo bado hakijatambulika na juhudi za kuuzima zinaendelea,
ambapo vikosi mbalimbali vya zimamoto vipo uwanjani hapo kuthibiti janga
hilo.
Uwanja huo hivi sasa umefungwa na hakuna ndege kutua ama kuruka isipokuwa kwa dharura tu.
Moto
huo unasemekana ulianza majira ya saa 11 za alfajiri sehemu za idara ya
uhamiaji na kusambaa katika eneo la abiria wa kimataifa.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya anaripotiwa kuelekea uwanjani hapo hivi sasa kukagua janga hilo, na habari
zinasema hakuna mtu aliyedhurika kwa moto huo ingawa hasara
iliyopatikana inasemekana ni kubwa na kwamba abiria wengi wamekwama
uwanjani hapo. Barabara kuu ya kuelekea JKIA imefungwa.
Tutaendelea kuwaletea habari zaidi kadri zitavyozidi kupatikana



No comments:
Post a Comment