Katika interview hii, wema sepetu ameongelea mambo mengi sana na
 makubwa yakiwema mapenzi, na maisha yake bunafsi kwa ujumla. Ifuatayo 
na sehemu ya interview hiyo kama iliyonukuliwa toka mtandao kwenye 
mtandao huo
Swali: Kuna wakati wowote uliwahi kujuta maisha ya ustaa baada ya kuwa Miss Tanzania?
Yes, nimewahi kujuta lakini mwisho wa siku huwaga nasema kwamba 
mwenyezi Mungu ndio anapanga kwasababu kama mwenyezi Mungu ndio 
amenipangia hivi nisingefika hapa kwanza, kwahiyo regrets zinatokea kwa 
kila mtu, lakini siwezi kusema kwamba zimetoka kwa mara nyingi, labda 
mara moja mara mbili na zinatokea pale tatizo linapotokea, hauwezi 
ukapata regrets kama hakuna tatizo.
Ukiwa staa kila mtu atataka awe rafiki yako, na kabla ya kuwa 
Miss Tanzania ni wazi ulikuwa na marafiki uliokuwa ukihang out nao hapa 
na pale, uliendelea kuwa na urafiki nao, ama baada ya kuingia maisha 
hayo ikakuwia vigumu kuwa nao tena pamoja?
Nina marafiki mpaka sasa ninahangout nao wanakuja mpaka nyumbani
 lakini hatushei sana zile common interests kama zamani because once 
upon a time tulikuwa tuko wote on the same rank. So nilivyokuwa nipo 
kwenye spotlight obvious nimekutana na watu wengine wapya watu ambao 
naonana nao katika kazi zangu za kila siku, because apart from being 
Miss Tanzania, I am also an actress, kwahiyo nakutana na wasanii wengine
 ambao labda nakaa nao kwa muda mrefu sana kwahiyo utajikuta tu unashare
 nao common interests sababu unafanya nao kazi pamoja.
Swali: Ulikuwa na boyfriend tayari?
Yes nilikuwa naye
Swali: Kuna wakati wowote aliwahi kujihisi inferior kutokana wewe kuwa maarufu? Ulifanyaje kumweka sawa?
Well, si unajua zile za kishuleshule, zile za kitoto naweza 
kusema. Sana sana ukishafika ile o-level nini utakuwa na yule boyfriend 
ambaye unaamka tu asubuhi umeshavaa unasema sasa hivi naenda kuonana na 
boyfriend wangu, ukisharudi kutoka shuleni from there nyumbani, no 
boyfriend. Yeah nilikuwa naye, in the beginning alivyojua kwamba 
nashiriki Miss Dar Indian Ocean akaniambia kwamba ‘ukishiriki mimi 
nisahau, sitaweza kuwa na wewe tena’, nikamwambia, why? Akaniambia 
‘utakuwa upo kwenye public’ nikamwambia ‘okay fine’, nikamdanganya 
kwamba sishiriki.
So siku moja gazeti la Mwananchi pale katikati kulikuwa na picha
 yangu kubwa ‘Miss Dar Indian Ocean kushindana kesho’ and lile gazeti 
kuanzia naingia shuleni naingia kila mtu ananiambia ameniona kwenye 
gazeti. So kitu cha kwanza nikafikiria ‘Mungu wangu yule mtu akiliona’ 
so sikuonana naye the whole day.
Nikiwa nyumbani ndio nikamuona anakuja kalishikilia, nikawa 
namsikiliza. Akaniambia, ‘nimeona gazeti lako and ndio hivyo kwahiyo 
umeshanidhihirishia kwamba umechagua hiyo issue, so fine we endelea’. 
Basi nikajaribisha kuongea naye lakini hakuweza kunisikiliza lakini 
luckily the next day wakati ndio nashiriki nimekaa pale time ya kujibu 
swali namuona pale anapiga picha kwahiyo he was there na alinisupport 
mpaka nilipofika Miss Tanzania lakini after that sababu nilikuwa 
ambassador wa Vodacom nikawa nafanya kazi Vodacom nikawa sionani naye 
vile kama kawaida, kila akinipigia simu nipo busy, yeye mwenyewe akasema
 tu ‘bwana mimi siwezi’. Basi tulielewana vizuri na mpaka kesho 
tunaongea, tunasalimiana’
Swali: Uwewahi kusema bila Kanumba usingeingia kwenye movies, marehemu alikuwa ana mchango gani kwako?
Nakumbuka nilipokutana na marehemu nilikuwa niko na dada yangu 
mimi nilikuwa nakaa na dada yangu, kwasababu once nilishawahi kuishi na 
mama yangu and then from there unajua baada ya kuingia kwenye nini nini 
nikawa busy. Dada yangu mimi kaolewa lakini kwa dada yangu nilikawa 
nahisi kama pako free zaidi, kwamba mama ukirudi ‘umetoka wapi sijui 
nini na nini hivyo, alikuwa haelewi. So ikabidi tu nianze kuishi na dada
 yangu.
Kwahiyo dada yangu akawa ananielewa, kwasababu hayupo sana 
protective kama mama. Siku hiyo tunabadilisha seating arrangement ya 
pale nyumbani kwa dada yangu tukawa tunatafuta carpet like different 
furnitures, so tukawa tumeenda hapa kulikuwa na hili duka kubwa hivi la 
Mwanamboka kulikuwa kuna furniture center, Pentagon, so tukawa tumeenda 
pale wakati tunaenda tulimkuta Kanumba wapo nje wameweka makamera yao 
nini ,wanashoot Lost Twins. So sisi tumeingia tunaona tu makamera, 
tumepark gari tumeingia ndani tunaangalia furniture. Akatokea Maya 
tukasalimiana akaniambia, ‘ jamani nakupenda’ na mimi nikamwambia na 
mimi napenda unavyoigiza’ nini na nini.
Tukatoka nje tukakutana tena na Maya akaniambia ‘jamani jamani kama unaweza pita kidogo tu hata uonekane, hata usalimie’.
Nikamwambia siwezi kwasababu nipo kwenye mkataba, akina Uncle 
Hashimu wataniua wakiniona nimefanya kazi au nimetokea kwenye nini bila 
kuwaconsult so akaniambia ‘basi sawa tuachie namba yako’. Wakati 
ananiambia tuachie nambo yako, Kanumba huyo anapita, ‘Kaka kaka ngoja 
umemuona Wema?’ Aliniringia sana.
‘Mambo’ nikamwambia ‘fresh vipi’ ‘safi’ nikamwambia poa,’Kaka 
basi chukua namba yake ya simu tunaweza baadaye like tunaweza tukamtumia
 kwenye movies’, ,Kanumba akamwambia achukue simu yake ndani. Basi 
nikamwangalia mimi mwenyewe basi ndio ninamwona mara ya kwanza, ‘Hee 
Kanumba’, kwasababu nimeangalia sana michezo yao.
Basi, so baada ya hapo akaleta akachukua namba yangu akanibeep 
nikamsave, basi mimi nikaondoka zangu. Sijafika mbali naona namba 
inanipigia ambayo nimeisave vilevile Steven Kanumba, nikapokea ‘Hello’ 
akaniambia ‘vipi, safi Kanumba hapa’ nikamwambia ‘namba yako nimeisave’ 
‘haya basi sawa basi baadae’ nikamwambia ‘poa’.
Mara like jioni jioni hivi akaanza kunitext ‘mambo’ ‘Safi’ ‘vipi
 uko wapi?. Basi kila siku tukawa tumejengeana tabia ya kutextiana kila 
siku tunandelea for one weak tunatext mara yeye ataniuliza umekula nini,
 mara sijui nini, obvious kwa mwanamke unakua tu unajua kwamba mwanaume 
akiwa ana interest na wewe. Kidogo tukaanza kuulizana una boyfriend una 
girlfriend sijui nini, hivyo. Akaniambia mimi ‘nipo kambini Lamada’ 
akanielekeza nikafika.
Basi nimefika siku hiyo tumekaa pale garden akaniambia 
ananipenda na nini, hivyo. Kipindi hicho nilikuwa sina boyfriend 
nilikuwa very very single, so nikamdanganya nikamwambia ‘mimi na 
boyfriend wangu sijui nini’ akaniambia ‘naomba tu just like nifikirie 
basi’ Nakumbuka tulivyokuwa tunaondoka ndo tukakiss, it was our first 
kiss. Basi nikaondoka, akaniambia ‘unaweza kurudi tena nikamwambia 
siwezi akaniambia please, please naomba urudi tena unikiss’ nikamwambia 
‘sawa’ basi nikarudi then akaniambia ‘l love you, love you too, mapenzi 
yakaanza.
Basi kwenye mapenzi yetu ndo akaniambia like ‘nataka kuact 
movies na wewe’ nikamwambia ‘mimi siwezi kuact’ akaniambia ‘mimi nahisi 
unaweza kuact hujajua tu’ nikamwabia sijawai kufikiria kuact, akaniambia
 ‘unaweza kulia’, nikamwambia ‘nilie nina sababu gani ya kulia’ 
akaniambia ‘basi kama huwezi kulia tutakumenyea vitunguu, ‘vitunguu 
ukimenya si unalia, basi tutakuwa tuna kumenyea vitunguu’ .
Akaniambia niende kuonana na bosi wake. Nilivyofika tu ofisini 
nikaonana na Mtitu Game. Akanipa script akaniambia nikasome kama story 
akaniambia ‘wakati unasoma uwe unasoma sana concentrate kwenye Dina. 
Basi vile tukiwa tukikutana tunafanya mazoezi nini, akaniambia ‘sawa 
basi wewe you are ready to shoot. Nilivyo shoot movie yangu kwanza, 
hauwezi amini, I just felt yaani kwanza niliona iko very easy. Kwa 
wengine wanaona it’s hard unajua.
Baada ya hapo ndo nilikuwa tayari nimetoa taji, I had to go back
 to school. Nikasafiri nikaelekea Malaysia kufanya kozi yangu ya mwaka 
ya International Business, wakati niko Malaysia nikatumiwa movie yangu 
ya Point of No Return. Tumekaa tunaangalia na marafiki zangu nikaona 
kwamba kumbe it’s nice, it’s fun. Nikampigia simu, ‘narudi for likizo 
soon naomba uniandalie script nataka ni shoot movie nyingine’
Nimerudi kweli ndo tukashoot Red Valentine, Family Tears, White 
Maria yaani tukashoot movie movie nyingi hivi so from there nikawa 
nimeshajikuta katika movie, so that why I keep saying kwamba without him
 nisingejua.
Swali: Hebu tuzungumzie uhusiano wako na Diamond ambao katika Swali: mahusiano yako yote ndio ulioandikwa zaidi kwenye magazeti, unakumbuka mlikutana wapi?
Mi na Diamond tuliwahi kukutana mara moja tu Billcanaz na 
hatukuwahi kusalimiana kabla ya kuanza uhusiano lakini tulikuwa 
tunaangalia sana, so nakumbuka alikuwa yupo smoking room kwahiyo tukawa 
tumepeana migongo, nilikuwa na rafiki zangu wawili. Nikamuona akaniona 
yeye alikuwa na rafiki yake, hatujasaliamija hatujafanya chochote mimi 
nimechukua vinywaji tukatoka nje na marafiki zangu tumesimama hapo nje 
nikawa naambiwa ‘yule ndio ameimba Kamwambie’ kipindi hicho nilikuwa 
namuona wa ajabu sana ila tu alijiseksisha kiasi fulani (kicheko 
kirefu).
Kipindi hicho mimi nilikuwa natoka na Chaz Baba so nakumbuka 
hiyo ndio ilikuwa the first and last day tumeonana. Mimi nikasafiri 
nikaenda Marekani, nilipofika kipindi hicho Kamwambie ndio ilikuwa hot 
na Mbagala ndio karelease. Dada zangu walikuwa wanampenda sana Diamond 
yaani just from the songs. Dada yangu wa kwanza ana miaka 14 yupo 
Marekani na hajawahi kurudi Bongo toka aondoke kwahiyo alikuwa anaona 
Bongo inafanya vizuri sasa hivi akaniuliza kama tuna urafiki na Diamond 
nikasema sio sana tunajuana tu.
Akaniambia nimwambia aende Marekani kufanya show sababu kila 
party tuliyokuwa tunaenda lazima watapiga Kamwambie halafu kila mtu 
anaipenda. So watu wakaanza kuniambia like ‘hebu find contact naye huku 
kuna mapromoter aje kufanya show’na kipindi hicho Profesa ndio alikuwa 
amekuja nikamwambia basi sawa mi nitamtafuta.
Nikamwabia Da Rehema, Ray C anitafutie contact zake. So siku 
moja nikaona anaplan kwenda kufanya show London, nika mclick Diamond 
Platnumz nikamtext, nikamwambia ‘hey mambo vp mzima upo London’ 
akaniambia ‘No mamie sipo London sijui ni nini’ nikamwabia ‘anyways Wema
 hapa nipo Marekani halafu it happens una fans wengi, akaniambia basi 
sawa acha nimalize issue ya London halafu nitakuambia.
Basi tukajenga tu mazoea tukawa tunachat nini yaani ikawa yeye 
anaingia Facebook kuchat na mimi naingia kuchat naye, washkaji tu yaani.
 Akawa ananiambia ‘bado uko na Chaz na nini’ nikamwambia yeah nipo na 
Chaz. Sasa ilikuwa ni kama mwezi wa nane wa tisa kama sikosei. Mimi 
wakati nipo Marekani nilikuwa naambiwa sana news kuhusu Chaz, mara Chaz 
sijui yupo na mwanamke gani, hiyo hiyo Facebook watu wananitumia mpaka 
picha nikumuuliza anakataa.
Sasa mimi nakumbuka dada yangu alikuwa anampenda sana Chaz so 
siku ya siku amekutana naye yupo sijui na mwanamke gani alipoaniambia 
nikasema, basi. So nikajikuta namuelezea matatizo Diamond. Siku 
niliyoamua kabisa mimi and Chaz are done nikamwambia mimi siwezi. So 
tukawa tunawasiliana na Naseeb hivyo. Siku moja tukanuniana, alikuwa 
amealikwa Ikulu halafu nikawa namtext hajibu, nikimpigia simu hapokei 
akaja akatoka akanipigia simu nikawa sijibu. Akanitumia meseji ‘baby I 
am sorry, we ndio faraja yangu sijui ni nini…. I LOVE YOU. Sikuona kitu 
kingine chochote nikaona tu hiyo. Basi nami nikamjibu sawa nimekusamehe 
lakini sijakusamehe sana, nimekusame kidogo. Akaniambia ‘niambie kitu 
kizuri’ na mimi nikamwambia I LOVE YOU. Basi akaniambia ‘mwenzio 
nakupenda, nachanganyikiwa’ basi no mapenzi yakaanza hapo.So niliporudi 
kutoka Marekani mimi na Naseeb tukaanza kuishi pamoja.
Swali: Mwaka jana alipooenda kutumbuiza kwenye Big 
Brother Africa, alidai kuwa ameweza kuongea Kiingereza kwasababu yako, 
ulikuwa ukimfundisha ama ulikuwa ukipenda kumuongelesha Kiingereza 
zaidi?
Yes. Naseeb alikuwa hajui Kiingereza, alikuwa anajua cha juu 
juu. Ila mimi na Naseeb tumekaa pamoja mwaka mzima kama mke na mume. So 
mimi nilivyo kidogo nimetupia Kiingereza kwahiyo hiyo ilikuwa inampa 
tabu kwenye the first two months kwahiyo most of the times nikawa 
naongea naye Kiingereza. Lakini he is smart, Naseeb is very smart yaani 
akiwa haelewi kitu ‘hivi baby hapa kwenye has na have unafanya nini, 
hapa natumia tense gani? Niweke ing niweke nini?’ mwisho wa siku 
nikajikuta like tunatumia most of the time kufundishana. Akisema kitu 
ambacho sicho namwambia ‘usije ukarudia tena kusema hivyo mbele za watu 
watakucheka’. So akajikuta tu anaweza.
Kwanini mliachana?
Mimi na Naseeb tuliachana baada ya yeye kunicheat na Jokate 
.Nilikuwa sijui and maisha yangu yote tangia nimeanza mapenzi na Naseeb 
naweza kusema kuwa sikuwahi kuwa unfaithful. I used to be very faithful 
to him na tulikuwa tunapendana sana. With Naseeb nilikuwa nimesharidhika
 na maisha ambayo niko nayo na hata kama yalikuwa not good, whatever 
lakini tayari nilikuwa nipo satisfied with me and him nilikuwa tayari 
nimesharidhika naye.
Nadhani pia inacost mwanaume akishajua kwamba anakutawala in one
 way or another so labda ni shetani au ni ibilisi alimuingilia baada ya 
kutaka kuanza kushoot video ya Mawazo ndo rumors zilianza, nikawa 
siamini kwanza. Siku moja ndio nikapigiwa simu na rafiki yangu anafanya 
kazi Piccolo akaniambia ‘Diamond yuko hapa na Jokate na wanakiss’. 
Nilitoka, nikachukua taxi nikaenda mpaka Piccolo, kitu cha kwanza 
niliona gari yake. Nilivyofika nikawakuta sijui wamewekeana miguu. 
Nilivyofika pale nikawasalimia wakawa wako kimya na nimeona ile kitu 
nikawaaga nikaondoka zangu. Nikaliaaaa, amerudi wakati huo bado tunaishi
 pamoja akanikutana napanga nguo, hakutaka kuongea sikutaka kuongea, 
tukachuniana, sikulala mimi na Naseeb kitandani for one week. Anaiona 
ile hali lakini hataki kuanza. Nikachoka, nikaja tu siku nimepanga nguo 
zangu nikaenda kwa dada yangu ndio ikawa kimoja. Basi mimi nikamwacha 
akaendelea na maisha yake na mimi nikaendelea na maisha yangu.
Swali: Unamiss chochote kutoka kwake?
Normally inakuaga ni ngumu sana kuadjust kwa maisha mapya. It’s 
always very hard kuanza tena love life sababu apart from mapenzi kuna 
kuna mazoea so inakuaga ngumu sana at the beginning. Nilikuwa, lakini 
not anymore sasa hivi naona kawaida tu kama tulivyoachana na wengine. 
Silook back nikamiss chochote, everybody is happy now.
Swali: Hivi majuzi yeye na mpenzi wake wa sasa Penny 
walikurekodi baada ya wewe kumpigia simu Diamond, ni kwa kiasi gani 
tukio hilo lilikuvunja moyo wako?
Sikuwahi kudhani kwamba Naseeb ni mtu wa aina hiyo kufanya kitu 
alichokifanya. Though nimesema kwamba nitaacha kama ilivyo na 
nisingependa kuiongolea lakini nilikuwa very disappointed, very very 
disappointed.
Swali: Ni kweli lilisababisha utamani kufa ama kulikuwa na jambo jingine?
Maneno yalikuwa mengi sana halafu ilivyotokea nilijipa moyo, 
‘you know what’ F it, bullshit ni mshenzi tu, mshamba tu ambaye hajaenda
 shule. Lakini kitu ambacho kilinifanya niwe torn ni the next day baada 
ya kuona post ambayo wanasema kwamba ni fake ya Diva, alitukana tukana 
sana, that was kitu kilichonifanya niwe like okay…… Lakini with the 
support and help ya watu ambao wananisurround, my family friends, the 
people who love me, wakanipa moyo.
Swali: Je! Ni sababu ya wewe kwenda vacation Arusha?
Yeah. My manager alinifanyia hivyo just to easy me up for whatever that imetokea.
Swali: Penny alikuwa rafiki yaki tangu utotoni, unahisi alikuzunguka kwa Diamond?
It’s a free world, kila mmoja ana uhuru wake wa kuishi 
anavyotaka yeye. They met, they fall in love wameanza mapenzi, mtu 
yoyote anaweza kufall in love na mtu yeyote asiwe questioned. Love 
doesn’t ask why, haiulizi kwanini, because alikuwa rafiki yangu then I 
can’t NO. Wapendana, I wish them all the best. Mimi na Penny si kwamba 
hatuongei sio sababu ya hii issue, tuna drama zetu tu za huko nyuma 
kwahiyo hii issue ni muendelezo tu.
Swali: Una nyumba yenye thamani ya milioni 400…
Sio shilingi milioni mia nne ni milioni 280. Milioni 400 watu 
wameniquote vibaya because Zamaradi aliniuliza ‘your empire ina worth 
kama shilingi ngapi’ ndio nikasema about… so nyumba no, niliinclude 
nyumba na magari na nini.
Swali: Okay, gaari karibu milioni 80, ofisi yenye 
thamani ya takriban milioni 70, uliwanunulia Gucci na Vanny vitu vyenye 
thamani ya karibu milioni 6, ulimtolea Kajala milioni 13 na mengine 
mengine, hivi how rich are you Wema? Are you a millionaire?
No, I’m just a normal person, not a millionaire, not a billionaire; I’m just Wema trying to live life.
Swali: Kwa mtanzania suala la kutumia mamilioni kwaajili
 ya shopping kwa mbwa tu haliwaingi akilini haraka, Vanny na Gucci wana 
thamani gani kwako mpaka uwagharamikie hivyo?
Vanny na Gucci are my everything. They are my everything because
 Wema Sepetu hana watoto, sina mtoto ila nawish kuwa na mtoto Inshallah 
mwenyezi Mungu akinijaalia nikapata uwezo wa kubear mtoto nitafurahi. 
Bado nadhani mpaka mwenyezi Mungu akinipa hiyo blessing ya kuwa na 
mtoto. Since then sina, so nawachukulia Vanny na Gucci kama watoto 
wangu, they are my babies. They are the reason mimi nikienda nyumbani 
niko stressed, they always make me smile. They are faithful, wako 
innocent; they are loyal hawawezi kunibetray, hawawezi kunihurt in 
anyway. Vanny akiumwa au Gucci nikimuona hayuko sawa I go crazy mpaka 
huwaga nalia. Tayari wana connection na mimi ambayo siwezi kuifananisha 
na kitu chochote. So they are my world. Kwahiyo mtu akitaka kumess na 
mimi amess na mbwa wangu hakutakalika I swear, I can do anything for 
those creatures, I can give my all for them.
Swali: Kitu gani ambacho ungependa watanzania wakifahamu kuhusu wewe ambacho unahisi wanapotoshwa?
The fact that wanavyosema mimi napenda scandal, mimi sipendi 
scandal , sipendi, hakuna binadamu anayependa scandal. I live to what 
makes me happy and kukifanya siogopi labda ndio kitu ambacho kinanicost.
 Naweza kusema kuwa kitendo cha mimi kuwavalisha nguo mbwa wangu 
kimewashangaza wengi lakini it makes me happy. If I look at them wako 
cute, wamependeza na sio nguo za binadamu zile ni nguo za mbwa kabisa 
ziko designed for dogs, ni viatu vya mbwa ambavyo viko designed for 
dogs, I can afford it, why not getting for my dogs, it makes me happy I 
live to it. Naweza kusema kwamba the fact ya mimi kuishi vile, roho 
yangu inapenda ndio inayonicost. Niko na mtu fulani, I want to make him 
be public kwa watu kwanini wasimjue, it makes me happy, I do it 
inanicost, ‘Wema Malaya sijui nini’ ndio kinachonicost.
 
 
 
 
 
 
 

 
No comments:
Post a Comment