Na Mwandishi wetu:
TUKIO kubwa la kigaidi lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika
jengo la maduka makubwa na ya bei mbaya jijini Nairobi la Westgate,
limeelezwa kuwa liliongozwa na mwanamke raia wa Uingereza, Samantha
Lewthwaite.
Yafuatayo ni mambo kumi usiyoyajua juu yake.
Yafuatayo ni mambo kumi usiyoyajua juu yake.
1.
Samantha, mwenye umri wa miaka 29, ni mzaliwa wa Buckinghamshire,
Uingereza anayeelezewa na magaidi wa kundi la Al Shabaab kama mwanamke
mwenye akili nyingi, akiwa ni mama wa watoto watatu ambaye alikata
mawasiliano na familia yake baada ya kuhamia Kenya mwaka 2007.
2. Ripoti za kipolisi zinaonesha kuwa ni mkufunzi wa
wanawake wa kikundi hicho cha kigaidi wanaochukua mafunzo ya jihad, mke
wa zamani wa Germaine Lindsay, ambaye alijiua baada ya kuhusika na
shambulio la bomu kwenye treni ya chini ya ardhi jijini London, Julai 7,
2005.
3. Kwa mujibu wa nyaraka mbalimbali zinazoaminika
kuwa ni zake, ambazo zilitangazwa na Gazeti la Daily Mail la Uingereza,
mwanamke huyo anawalea watoto wake ili waje kuwa wanaharakati wa imani
kali. Mumewe wa pili, Habib Saleh Ghani naye ilidaiwa kuwa aliuawa
kwenye tukio lingine la ugaidi.
4. Baadhi ya nyaraka zinaonesha kuwa katika baadhi
ya mawasiliano na mumewe, aliwahi kusema: “Ghani alizungumza na kijana
wangu wa miaka nane na binti yangu wa miaka mitano akiwauliza
wanachotaka kuja kufanya wakiwa wakubwa, wana majibu mengi lakini wote
wanakubaliana kwamba watakuja kuwa Mujahidina.
5. Ni mtaalamu wa kutengeneza vifaa vya kuficha
sura, pua na kichwa, akiachana na taaluma yake ya zamani ya ubunifu wa
mitindo ya mavazi ambayo sasa anashona yanayovaliwa na Waislamu, kazi
aliyoianza akiwa chini ya uangalizi wa magaidi hao wakati akiishi
Mombasa nchini Kenya.
6. Anahisiwa kuwa ndiye aliyetupa guruneti katika
baa iliyokuwa imejaa mashabiki wa soka wakitazama mechi za Euro mwaka
2012 katika mechi kati ya England na Italia nchini Uganda Juni 24 na
kuua watu watatu, akiwemo mtoto aliyekuwa na umri wa miaka mitatu. Isack
Simiyu, (23), aliyekuwa nje ya Jericho Bar, alisema shambulio hilo
lilifanywa na mwanamke wa kizungu aliyejifunga kitambaa cheusi kichwani.
Alidai kumuona vizuri mlipuaji huyo na polisi walipompa picha nne za
wanawake wa kizungu ili aone kama mlipuaji alikuwa mmojawapo, aliichagua
ya Samantha.
7. Ni gaidi wa kike anayetisha zaidi kwa sasa tokea
alipoondoka Ulrike Meinhof, mwanzilishi wa Kundi la Red Army ambalo
lilihusika na milipuko ya mabomu katika Ujerumani Magharibi kwenye miaka
ya 1970.
8. Alipokimbia katika nyumba aliyokuwa amepanga
mjini Mombasa, polisi walikuta kitabu kidogo cha kumbukumbu akiwa
ameandika kuwa anataka watoto wake waje kuwa wakujitoa mhanga. Pia
walikuwa na bunduki za kisasa, risasi, pamoja na mapipa ya kemikali
yanayotumiwa na wanaojilipua.
9. Akiwa na jina la Kiislamu la Asmaa Shahidah
Bint-Andrews, kijana wake wa kiume, Abdur-Rahman Faheem Jamal, alizaliwa
katika Hospitali ya Stoke Mandeville mwaka 2009. Katika cheti cha
kuzaliwa cha mwanae, hakuna jina la baba lililoandikwa. Alislimu akiwa
na miaka 18, akiachana na uvaaji wa jeans na Tisheti na badala yake
akivaa mavazi ya Kiislamu, ikiwemo hijab.
10. Alisoma masomo ya dini na siasa katika shule
iitwayo Oriental and African Studies huko Russell Square, London, umbali
wa mtupo wa jiwe kutoka pale mumewe alipojiua kwa kujilipua.
CREDIT GLP
No comments:
Post a Comment