Azam TV inataraji kuwa hewani rasmi
katikati ya mwezi Novemba na kuzinduliwa rasmi mwishoni mwa mwezi ujao
huku ikianza na Channel zaidi ya 35 Bureee na baada ya uzinduzi mteja
atapata Channel 50+ kwa gharama nafuu ya 12,500/= tu kila mwezi. Azam Tv
wanasema wao hawana ubaguzi wateja wote ni sawa na hakuna package
maalum kwa watu maalum.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam TV, Rhys
Torrington akifafanua mambo kwa waandishi wa habari mbalimbali
waliofanya matembezi katika kituo hicho kipya cha habari za michezo na
burudani kilichopo Tazara jijini Dar es Salaam kujionea maandalizi ya
mwisho mwisho kabla ya kuanza kutrusha matangazo yake moja kwa moja. Kwa
sasa kituo hicho chenye mkataba wa kurusha live mechi zote za Ligi kuu
ya Soka Tanzania Bara kinarusha kupitia Televisheni ya Taifa, TBC.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam TV, Rhys Torrington akionesha kwa wanahabari Kisumbusi
Wanahabari walikuwa makini sana kufuatilia neno hadi neno
Ziara ilinza na hapa C.E.O wa Azam TV, Rhys Torrington aliwatembeza wadau
Hizi ni meza za Huduma kwa Wateja,
pindi wateja watakapofika AZAM TV kununua Visumbuzi vyao basi hapa ndipo
watapokelewa na kupata maelezo yote muhimu.
Hii ndio sehemu ya Huduma kwa Wateja na Mapokezi ya Azam TV. Ni maridadi na yakuvutia.
Ziara ilikuwa ya furaha sana.
hapa ni dawati la kupokea kero na utatuzi wa masuala mbalimbali ya Azam Tv hasa kupitia Kisumbuzi chake.
Hili ndo gari la kisasa na laaina yake la kurusha matangazo.
Ndani ya gari hilo kuna mitambo mingi sana.
Wana habari wakilamba picha na mtaalam wa Azam TV, Yahaya Mohamed.
Yahaya Mohamed akitoa somo la mitambo hiyo inavyoendeshwa.
Wanahabari wakipata somo
Waandishi wakiingia kwa OB van
No comments:
Post a Comment