Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
KOCHA Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, juzi Jumatano
alikuwa katika wakati mgumu na kulazimika kuzichapa na shabiki ambaye
alimvaa na kumtupia maneno makali.
Mashabiki akadhaa walimtuhumu kuchukua mlungula na kusababisha timu
hiyo kushindwa kufanya vizuri baada ya kuambulia suluhu katika mechi
dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Baada ya mechi hiyo mashabiki hao walimfuata Julio nyuma ya jukwaa
kubwa na kumzonga huku wakimtupia lawama kwa kuihujumu timu yao.
Julio alipoona mashabiki hao wanaendelea kumtolea lugha kali, naye
alikazana kuwajibu kwa kuwatolea lugha kali, baada ya mapishano kushika
kasi, Julio akitumia makabrasha aliyokuwa ameyashika, akaanza kumpiga
nayo shabiki mmoja kichwani.
Baada ya kuona vuta nikuvute imezidi
ndipo askari wa kutuliza ghasia waliitwa kutuliza zogo hilo ili kocha
huyo aondoke kwa amani uwanjani hapo.
“Wewe tushakujua mtu wa ‘ten percent’, huna lolote, unaacha
kuchezesha wachezaji wa maana unatuwekea makanyanga yako,” alisikika
shabiki huyo aliyetwangwa na makabrasha kichwani.
“Kwani we nani kwenye timu hii, hata kadi huna hapo ulipo,” alisikika
Julio akijibu mashambulizi huku akiingia kwenye gari aina ya Mitsubishi
Erandis yenye namba za usajili T 404 CBJ.
CREDIT GPL.
No comments:
Post a Comment