Waziri
wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo katikati akishirikiana na
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kulia kwake, Mbunge wa
Nkasi Kusini Ally Kessy kushoto kwake na wazee wawili kulia na kushoto
wakiwawakilisha wananchi wa Namanyere (Wilaya ya Nkasi) katika uzinduzi
rami wa mradi wa umeme kutoka Sumbawanga hadi Namanyere Wilayani Nkasi
leo tarehe 28, Oktoba 2013. Mradi huo uliogharamiwa na Serikali ya
Tanzania na kukamilika hivi karibuni una gharama ya Tsh. Bilioni 4.3 na
umepitia jumla ya vijiji kumi na mbili vya njiani kabla ya kutua
katika Mji huo wa Namanyere uliopo Wialayani Nkasi Mkoani Rukwa. Tangu
Tanzania ipate Uhuru mwaka 1961 na tangu kuundwa kwa Mkoa wa Rukwa mwaka
1974 Wilaya hiyo haikuwa na umeme jambo ambalo limepokelewa kwa shangwe
na wananchi wa Wilaya hiyo.
Waziri
wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na washirika wake katika
uzinduzi huo wakibofya kitufe maalum kama ishara ya kuwasha umeme katika
Mji wa Namanyere leo tarehe 28, Oktoba 2013 baada ya Wilaya hiyo kukosa
huduma hiyo katika kipindi chote cha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.
Katika uzinduzi huo Prof. Muhongo amesema Mkoa wa Rukwa umetengewa zaidi
ya Tsh. bilioni 30 kwa ajili ya umeme vijijini kupitia REA, Wakala wa
Umeme Vijijini ambapo jumla ya vijiji 66 katika kipindi cha miezi 20
ijayo kuanzia Novemba mwaka huu 2013 vitanufaika na mradi huo.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkaribisha Katibu Tawala
Mkoa huo Alhaj Salum Mohammed Chima kuwasalimia wananchi wa Kirando
katika ziara ya kikazi ya siku mbili ya Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter Muhongo Mkoani Rukwa. Katika ziara yake hiyo anatembelea
miradi mbalimbali ya umeme pamoja na kuzungumza na wananchi.
Meneja
Mahusiano wa Shirika la Umeme nchini TANESCO Bi. Badra Masoud
akisherehesha baadhi ya mambo katika hafla fupi ya uzinduzi wa mradi huo
uliofanyika Namanyere Wilayani Nkasi leo tarehe 28, Oktoba 2013.
Waziri wa Nishati na
Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongea na baadhi ya viongozi wa Serikali
ya Mkoa wa Rukwa na Wilaya ya Nkasi leo tarehe 28, Oktoba 2013 juu ya
upatikanaji wa umeme katika bandari mpya inayoendelea kujengwa ya Kipili
Wilayani humo. Alisema kupitia REA, Wakala wa umeme vijijini kuanzia
mwezi Desemba miradi mbalimbali itaanza kufanya kazi kuweza kufikisha
umeme katika maeneo tofauti Mkoani Rukwa ikiwemo bandari hiyo ya Kipili.
Waziri wa Nishati na
Madini Prof. Sospeter Muhongo akiwa ameshikilia kinyago cha mfano wa
mtoto na mmoja ya wanakikundi cha ngoma za asili cha Kanondo cha Mkoani
Rukwa baada ya kufurahishwa na uchezaji wa ngoma ya kikundi hicho
inayoelezea malezi bora kwa watoto.
Waziri
Muhongo katika mikutano yake na wananchi hakusita kuwainua Mameneja wa
Tanesco kuelezea juu ya miradi mbalimbali ya umeme Mkoani Rukwa. Kulia
ni Meneja wa Tanesco Kanda ya Nyanda za Juu Magharibi Bi. Salome
Nkondola na katikati ni Meneja wa Tanesco Mikoa ya Rukwa na Katavi.
Picha
ya pamoja kati ya Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na
baadhi ya viongozi wa chama na Serikali wa Mkoa wa Rukwa.
No comments:
Post a Comment