Wadau na mashabiki wa mastaa wawili nchini, Wema Sepetu wa Bongo
Movie na Nasibu Abdul ‘Diamond’ wa muziki wa kizazi kipya, wamebariki
ndoa ya wapenzi hao kwa kusema kuwa ni watu wanaoendana na kutegemeana
kwa kiasi kikubwa.

Mwanzoni
mwa wiki hii, Wema na Diamond walitupia katika kurasa zao za mitandao
ya kijamii picha zao, ambazo zinaonekana zilipigwa eneo moja kwa simu
moja na hivyo kuwapa wakati mzuri mashabiki wao ambao walionekana
kupendezwa na uhusiano wao na kupendekeza waoane.
“Hii ndiyo couple
bomba zaidi ya wasanii Bongo, kwa nini msioane? Mnapendeza sana jamani,
ebu Diamond Platnumz achana na Penny bwana, huendani naye kwanza kuna
mambo ya dini na nini…,” aliandika shabiki mmoja.

Mwingine
aliandika: “Nadhani Penny angejiweka tu pembeni awaache hawa wawili, ni
mastaa kwa fani zao, yeye angeendelea tu na kazi yake ya utangazaji.
Kwanza kwake ni maumivu tu kuwa na msanii ambaye ana shughuli nyingi za
kisanii, bora wale wenyewe wanajuana.”
Ingawa kwa muda mrefu Diamond
amekuwa akikanusha kurudiana na Wema, hivi karibuni picha zao zilivuja
katika mitandao ya kijamii wakiwa China wakila bata na alipoulizwa,
‘alizuga’ eti walikuwa wakitengeneza filamu.
Hata hivyo, uchunguzi wa
gazeti hili umebaini kuwa, wadau wengi wanaamini Wema na Diamond
wanapendana kwa dhati hivyo wakapendekeza wafunge ndoa na kuyaacha
maisha mengine yaendelee kuwepo kuliko kuachana kisha kurudiana mara kwa
mara.
CHANZO NI GLP
No comments:
Post a Comment