Wanafunzi wa kike wa Ikuwo sekondari kwa sasa wanalala hapa kama ilivyoshuhudiwa na mtandao huu.
kama kawaida wamepanga magodoro yao chini kwa raha zao
Mkuu wa shule ya Ikuwo Sekondari akifafanua jambo kwa mwandishi wetu.
=====
Na Edwin Moshi, Makete
Kutokana
na idadi ya wanafunzi wengi wa kike wilayani Makete mkoani Njombe
kukatisha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupata mimba, shule ya
sekondari Ikuwo imeonesha kukerwa na tatizo hilo na kuamua kuchukua
hatua za awali za kupambana nalo
Mwandishi
wa mtandao huu alifika shuleni hapo na kukuta wanafunzi wa kike wote
wakiwa wanalala shuleni hapo licha ya mabweni hayo kukumbwa na
changamoto ya ukosefu wa vitanda
Mkuu
wa shule hiyo akizungumza na mwandishi wetu amesema kutokana na tatizo
hilo kuzidi kuwa kubwa, uongozi wa shule na wilaya kwa ujumla
walikubaliana wanafunzi hao watandike magodoro sakafuni waendelee kulala
mabwenini humo, wakati serikali ikiendelea kutafuta vitanda kwa ajili
ya mabweni hayo
"Kwa
wakati huu ambao tunasubiri kuletewa vitanda na serikali, tumeona ni
bora wanafunzi hawa wa kike waendelee kulala chini kwa kutandika
matandiko yao ili kupunguza ukubwa wa kupata mimba pamoja na kufeli"
alisema mwalimu mkuu huyo
Mtandao
huu ulipenya kwenye mambweni hayo na kushuhudia magodoro yaliyotandikwa
kwa unadhifu wa hali ya juu, ambapo wanafunzi hao wanalala kwa muda
wakisubiria vitanda
Hivi
karibuni katika mahafali ya kidato cha nne Iwawa sekondari afisa elimu
sekondari wilaya ya Makete Jacob Meena alikaririwa akisisitiza wanafunzi
wa kike wa shule hiyo waanze kulala shuleni kuanzia mwakani hata kama
mabweni hayana vitanda kama wanavyofanya Ikuwo sekondari.
No comments:
Post a Comment