Meneja
masoko wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kanda ya kusini na mkoa
wa Morogoro Aminata Keita akikabidhi baadhi ya Vitabu vilivyotolewa na
kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa Salma Hamisi ambaye ni
mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Ilulu iliyopo mkoani Lindi. Airtel
ilitoa vitabu vyenye thamani ya shilingi Milioni tano kwa shule hiyo.
Meneja
masoko wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kanda ya kusini na mkoa
wa Morogoro Aminata Keita akimkabidhi Bernard Swai ambaye ni mwanafunzi
wa shule ya sekondari ya Chalinze. Airtel ilitoa vitabu vyenye thamani
ya shilingi milioni tano kwa shule hiyo.
Meneja
masoko wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kanda ya kusini na mkoa
wa Morogoro Aminata Keita akimkabidhi Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya
sekondari ya Chalinze iliyopo mkoani Pwani baadhi ya vitabu
vilivyotolewa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa shule ya
sekondari Chalinze. Wanaoshuhudia katikati ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo
Bw. Emmanuel Kahabi pamoja na msimamizi wa bodi ya shule hiyo Bw. Mzee
Madeni.
Meneja
masoko wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kanda ya kusini na mkoa
wa Morogoro Aminata Keita akiwaelekeza jambo watoto wa shule ya
sekondari Nanyamba iliyopo Mkoani Mtwara ikiwa ni muda mfupi baada ya
kampuni ya mitandao ya simu za mkononi Airtel kukabidhi vitabu vyenye
thamani ya shilingi milioni tano kwa shule hiyo ya sekondari.
No comments:
Post a Comment