PICHA za aliyekuwa mke wa marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ Wastara 
Juma akiwa na mwigizaji Bondi bin Salim ‘Bond’ zimezua utata ambao 
unakazia ukweli wa taarifa ya kuwa wawili hao ni wapenzi.

Kikizungumza
 na Ijumaa Wikienda chanzo chetu kilicho makini, kilisema kinawashangaa 
sana Wastara na mwenzi wake huyo kuukana upenzi wao kila kukicha wakati 
picha zinajieleza.

“Wastara
 amekuwa akimkana Bond kuwa si mpenzi wake ila ni kaka yake sasa hebu 
tazama picha zao mpya, hata mtoto mdogo humdanganyi kitu,” kilisema 
chanzo hicho huku wawili hao wakiendelea kukanusha kuwa na uhusiano wa 
kimapenzi.
 
No comments:
Post a Comment