Habari na Bin Zubeiry.
MSHAMBULIAJI
wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Makumbi Juma ‘Homa ya Jiji’
amewashauri viongozi wa klabu yake ya zamani, Yanga SC kuwashirikisha
wachezaji wake wa zamani katika uongozi ili kusaidia masuala ya
kitaalamu.
Akizungumza
na BIN ZUBEIRY jana, Makumbi aliyekuwa akifahamika pia kwa jina lingine
la utani kama Bonga Bonga alisema kwamba watu wenye fedha ni muhimu
katika klabu, lakini hata wataalamu ni muhimu pia.
Makumbi
amesema Yanga SC hivi sasa ina hali nzuri kiuchumi kutokana na kuwa na
viongozi wa wenye fedha kama Mwenyekiti wake Yussuf Manji na baadhi wa
Wajumbe kama Abdallah Bin Kleb, Seif Ahmed ‘Magari’, Mussa Katabaro na
Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga, lakini inakosa wataalamu wa masuala ya
kiufundi.
Pesa si kila kitu; Makumbi Juma akizungumza na BIN ZUBEIRY jana |
Amesema
Yanga ina utajiri mkubwa wa wataalamu, lakini viongozi wa klabu hiyo
wameshindwa kuutumia na ndiyo maana pamoja na utajiri wao wanakwama kuwa
na timu bora.
“Kuna
wachezaji wengi wa zamani wenye mapenzi na Yanga na ambao pia ni
wanachama, lakini hawashirikishwi na ndiyo maana timu inashindwa kufanya
vizuri. Lazima tushirikishwe kwa sababu sisi tunaujua mpira na
tumeucheza, wao wawezeshe mipango ya fedha, na sisi tutengeneze mambo ya
kitaaamu, mambo yawe mambo,”alisema Bonga.Wakali wa enzi hizo; Kutoka kulia Thomas Kipese, Paschal Kaliasa na Mohamed Hussein, wachezaji wa zamani wa Yanga SC |
Alisema;
“Hawataki kabisa kusikia wachezaji wa zamani wa Yanga katika mfumo wa
uongozi, hicho kitu siyo sawa, kuna mambo ambayo yanahitaji utaalamu,
lakini pia hata nidhamu ya wachezaji imekuwa mbovu kwa sababu hawajui
historia ya klabu wala magwiji wake,”.
“Leo
hii mchezaji wa Yanga hamjui hata Sunday Manara ni nani wala Mohamed
Huusein ni nani, kwa sababu viongozi hawathamini wachezaji wa zamani.
Mimi wakati nasajiliwa Yanga (miaka ya 1980) nilipoingia pale klabuni
nilikuta picha za wachezaji waliotutangulia akina Leonard Chitete,
Maulid Dilunga na wengine na vikosi pia, lakini leo ukiingia Yanga
hukuti hata picha ya kikosi cha msimu uliopita, haya ni makosa
sana,”alisema Bonga.
Bonga
amesema anawaheshimu viongozi wa Yanga, lakini lazima ufike wakati
waienzi historia ya timu na magwiji wake ndiyo hata wachezaji watakuwa
na nidhamu na kuithamini klabu.
“Leo
pale Yanga kuna wachezaji wanajiona wanacheza mpira mkubwa sana, lakini
ukweli ni kwamba hawajafikia uwezo wa wachezaji tuliowatangulia, ila
kwa sababu klabu haina kumbukumbu za wachezaji wa zamani, basi Yanga
inaonekana timu ya leo leo tu,”alisema.
Hoja
za Makumbi ziliungwa mkono na wachezaji wengine wa zamani wa Yanga,
washambuliaji Thomas Kipese ‘’Ucle Thom na Mohamed Hussein ‘Mmachinga’
ambao walimalizia soka yao kwa mahasimu, Simba SC aliokuwa wakati
anazungumza.
“Haya
anayozungumza Bonga ni ukweli kabisa,”alisema Uncle Thom. “Lazima
viongozi wa Yanga wawashirikishe wachezaji wa zamani, hata sisi
tulipoingia pale Yanga tuliwakuta wachezaji wa zamani katika mfumo wa
uongozi, kwa nini leo hawapo?”alihoji Mmachinga.
No comments:
Post a Comment