SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limemuajiri Katibu wa zamani wa klabu ya Yanga
SC, Celestine Mwesigwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa shirishiko hilo.
Taarifa
ya Rais wa TFF, Jamal Malinzi imesema kwamba, Mwesigwa amekidhi sifa za
nafasi hiyo, akiwa na kiwango cha elimu ya Shahaha ya Uhusiano wa
Kimataifa na Stashahada ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Aidha,
TFF pia imemuajiri katibu wa Simba SC, Wakili Evodius Mtawala kuwa
Mkurugenzi wa Vyama na Masuala ya Kisheria ya TFF- ambaye ana Shahada ya
Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pia na Shahada ya Uzamili ya
uongozi wa Biashara ya Chuo Kikuu cha ESAMI.
Malinzi
amesema, Iddi Mshangama atakaimu ya nafasi ya Mkurugenzi wa Mashindano
ya TFF, iliyokuwa inashikiliwa na Saad Kawemba, wakati Danny Msangi
atakaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Fedha na Utawala TFF na Boniphace
Wambura Mgoyo ataendelea kuwa Ofisa Habari wa shirikisho.
Malinzi
aliyesema ajira zote zitaanza rasmi Januari 1 mwakani, pia ameteua
Kamati tatu, ya Uchaguzi, Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF nay a Soka
ya Ufukweni.
Kamati
ya Uchaguzi itakuwa chini ya Mwenyekiti, Wakili Melchesedek Lutema,
Makamu wake Wakili Walter Chipeta na Wajumbe Hamidu Mahmoud Omar,
Jeremiah John Wambura na Hassan Daalal.
Kamati
ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF itakuwa chini ya Mwenyekiti Wakili Julius
Lugaziya, Makamu wake Wakili Mwita Mwaisaka na Wajumbe Juma Abeid
Khamis, Rashid Dilunga na Masoud Issangu, wakati Kamati ya Soka ya
Ufukweni itakuwa chini ya Mwenyekiti Ahmed Mgoyi na Wajumbe Deo Lucas,
Juma Mgunda, Boniphace Pawasa, Joseph Kanakamfumu na John Mwansasu.
No comments:
Post a Comment