Mtangazaji
wa kipindi cha Mboni show, Mboni Masimba akimkabidhi zawadi mtoto
yatima Ally Mustapha baada ya kuimba vizuri katika mlo uliandaliwa na
Mboni katika ukumbi wa Highland hall.
Wageni
katika hafla maalum ya mlo wa pamoja uliondaliwa na kipindi cha Mboni
Show, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi
(kulia), Mboni Masimba katikati akiwa na mkurugenzi wa makampuni ya
Asas, Salim Asas Abri, mgeni kutoka Nigeria
Na Denis Mlowe wa Francis Godwin Blog
MTANGAZAJI wa kipindi cha ‘Mboni Show’ kinachorushwa na luninga ya EATV, Mboni Masimba siku ya jana amejumuika pamoja katika hafla na watoto yatima zaidi ya 200 walioko katika mkoa wa Iringa.
MTANGAZAJI wa kipindi cha ‘Mboni Show’ kinachorushwa na luninga ya EATV, Mboni Masimba siku ya jana amejumuika pamoja katika hafla na watoto yatima zaidi ya 200 walioko katika mkoa wa Iringa.
Katika hafla hiyo umejumuisha vituo vitatu
vya watoto yatima vilivyoko mkoani Iringa vya Upendo center na
Tosamaganga na kingine kilichoko katika wilaya ya Mufindi cha Moyo kwa
Moyo.
Hafla hiyo ya kula chakula cha mchana
na yatima imefanyika katika ukumbi wa Highland hall na kuhudhuriwa na
baadhi ya wafanyabiashara maarufu mkoani hapa akiwemo mkurugenzi wa
makampuni ya Asas, Salim Abri Asas na mgeni rasmi alikuwa kamanda wa
Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi..
Mbali ya kuwalisha watoto hao mboni ametumia muda huwa kuendesha kipindi chake cha Mboni Show kwaa kujumuika na watoto hao.
Mbali ya kuwalisha watoto hao mboni ametumia muda huwa kuendesha kipindi chake cha Mboni Show kwaa kujumuika na watoto hao.
Watoto yatima hao walipata zawadi mbalimbali ambazo zimetolewa na Mboni.
Mtangazaji huyo amekuwa ni mmoja wa watangazaji wanaojitolewa kwa kiasi kikubwa katika kusaidia watoto yatima na kufikia hatua wakati mwengine kuangusha kilio kutokana na kubanwa na huzuni kutoka kwa watoto hao.

Mboni alisema lengo kuu ni kuwakumbusha
watanzania juu ya kuwakumbuka watoto yatima kama ambavyo wamekuwa
wakichangia sherehe mbali mbali kama harusi, vipaimara, na kitchen
party.
No comments:
Post a Comment