Mwimbaji
wa muziki wa injili Solomon Mahlangu kutoka nchini Afrka Kusini akiimba
jukwaani kwenye uwanja wa Taifa katika tamasha kubwa la Krismas
lililofanyika jijini Dar es salaam likishirikisha waimbaji wengi kutoka
nchi mbalimbali za afrika wakiwemo waimbaji wa Tanzania, Mwimbaji huyo
Nguli wa muziki wa njili ameonyesha uzoefu mkubwa katika kuimba tofauti
na waimbaji wengine waliotangulia ukiacha Ephraim Sekereti wa Zambia,
kutokana na kuimba nyimbo mbalimbali za kizuru kiingereza na kiswahili
kwa ufasaha.
Mgeni
rasmi Waziri wa nchi katika ofisi ya waziri mkuu Uratibu wa Sera na
Bunge Mh. William Lukuvi akizungumza katika tamasha hilo na kuwashukuru
waimbaji wa muziki wa injili kwa kuendelea kuhubiri amani nchini lakini
pia akawahakikishia kwamba serikali kitahakikisha amani iliyopo inadumu,
kulia ni mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama na katikati ni
Ezekiel Maige Mbunge wa jimbo la Msalala hivi punde atapanda jukwaani
mwimbaji nguli wa muziki huo kutoka nchini Afrika Kusini Solomon
Mahlangu ili kuhitimisha tamasha hilo kwa jiji la Dar es salaam.
Mwimbaji
Ephraim Sekereti akitumbuiza kwenye uwanja wa Taifa wakati wa tamasha
la Krismasi linaloandaliwa na kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar
es salaam.
Mwimbaji
wa muziki wa injili Boni Mwaiteje akipagawisha mashabiki wake wakati
akitumbuiza kwenye Tamasha la Krismas linaloandaliwa na kampuni ya Msama
Promotion ya jijini Dar es salaam kwenye uwanja wa Taifa, katika tamash
hili pia yuko mwimbaji nguli wa muziki huo kutoka nchini Afrika Kusini
Solomon Mahlangu.
PICHA ZOTE NA FULL SHANGWE BLOG
No comments:
Post a Comment