EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, December 19, 2013

Polisi waua raia watatu kwa risasi

  Walikwenda kuwatoa wenzao waliokamatwa kwa mauaji
  Wenzao wachoma kituo, gari la polisi, pikipiki, majadala ya kesi
Mkuu wa jeshi la Polisi nchini,(IGP) Said Mwema
Watu watatu wameuawa kwa kupigwa risasi na askari wa Jeshi la Polisi wa Kituo cha Malinyi Wilaya ya Ulanga mkoani hapa, na wengine kujeruhiwa vibaya.

Tukio hilo lilitokea jana asubuhi baada ya  kundi la wakazi wa Kijiji cha Igawa   kuvamia kituo hicho wakitaka kuwatoa  wenzao waliokamatwa kwa tuhuma za mauaji.
Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu,  Diwani wa Kata ya Malinyi, Said Tilla, alisema tukio hilo lilitokea jana majira ya asubuhi baada ya wakazi hao wakiwamo waliouawa na kujeruhiwa kuvamia kituo hicho.

  Tilla, alisema kundi la wakazi hao waliandamana hadi katika kituo hicho   wakiwa na matawi ya miti kushinikiza kutolewa kwa wenzao hao walikamatwa siku mbili zilizopita kwa madai ya kumua mfugaji wa jamii ya Kisukuma, Matanji Luhembe (16).

  Alisema kitendo cha wakazi hao  kuvamia kituo hicho kinatokana na askari wake  kuwakamata wakulima hao watatu peke yao na kuwaacha wafugaji jamii ya Kisukuma wakati wao ndiyo chanzo cha mapigano hayo.

 Wafugaji hao wanadaiwa kumuua mjumbe wa kamati ya mazingira ya kijiji hicho, Victory Maleka Desemba 12, mwaka huu.

Alisema wakazi hao  walipofika katika kituo hicho, waliwakuta askari saba    wakiendelea na kazi baada ya kuzidiwa  waliamua kuwapiga risasi za moto na kuua  watatu na kujeruhi wengine wanne  kisha kukimbilia kusikojulikana.

“Wananchi hawakuwa na siraha zozote bali walikuwa na matawi tu ya miti, walipofika na kutaka wenzao watolewe ndipo askari wakaanza kupiga risasi ovyo na kuwaua watu watatu papo hapo na wengine kujeruhiwa na kisha hao askari wakakimbia na kutelekeza kituo hicho,” alisema Diwani Tilla kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Aliwataja waliouawa kwa kupigwa risasi  kuwa ni Leon Chikwale, Andrew Kikonoki na Edson Kidunde, wakazi wa kijiji hicho.

Alisema majeruhi hao walikimbizwa  Hospitali ya Misheni ya Lugala kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.

Diwani huyo, alisema baada ya  mauaji, wakazi hao waliamua kuchoma moto kituo hicho, na gari la polisi na pikipiki za kituo hicho huku baiskeli zilizokamatwa katika matukio mbalimbali wakizichoma pia.

Hata hivyo,  alisema katika tukio hilo hakuna askari yoyote aliyejeruhiwa na wakazi hao na kwamba Jeshi la Polisi limeamua kuongeza nguvu ya askari kutoka sehemu mbalimbali ikiwamo wilaya ya Kilombero na mkoa wa Morogoro ili kutuliza ghasia hizo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Furaha Lilongeri, alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo yaliyosababishwa na askari hao kuwapiga raia watatu waliokuwa miongoni mwa wananchi waliovamia kituo cha polisi.

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Faustine, Shilogile, alithibitisha kutokea kwa mauaji ya watu hao papo hapo  na wengine kujeruhiwa baada ya kutokea  mapambano baina yao.

Shilogile alisema watu hao waliouawa ni kati ya zaidi ya wakazi 500 wa kijiji  waliovamia kituo hicho wakishinikiza kutolewa kwa wenzao wanne waliokamatwa kwa tuhuma za  mauaji ya watu wawili na kuchoma moto nyumba saba.

Alisema polisi walilazimika kutumia nguvu kuwatawanya wakazi hao waliovamia kituo kwa nia ya kutaka kukichoma moto.

Kamanda huyo,  alisema wakazi hao walichoma  moto gari la askari aina ya Pick up, pikipiki ya polisi, baiskeli tano  za vielelezo na majalada ya kesi  yaliyokuwamo kituoni hapo .

Alisema wakazi hao walivamia kituo hicho kwa nia ya kuwatoa watuhumiwa wanne waliokamatwa usiku wa Desemba 14, mwaka huu kwa tuhuma za mauaji ya watu hao wawili, lakini  wakati tukio hilo likiendelea,   walikuwa  wameshahamishiwa kituo kingine cha polisi.

Alisema majeruhi  wanne wa tukio hilo wamekimbizwa Hospitali ya Lugalo kwa matibabu zaidi huku jeshi hili likiongeza nguvu kutuliza ghasia hizo.

Tukio la kuuawa mfugaji huyo na kusababisha watu wannne kukamatwa lilitokea Desemba 13, mwaka huu baada wafugaji wa jamii ya Kisumuma kumpiga na kumjeruhi vibaya hadi kumuua Victory Maleka (55).

Chanzo cha kifo cha Maleka ni wafugaji wa Kisukuma kumtuhumu marehemu kuwaelekeza askari wa wanyamapori wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) maeneo wanayoishi wafugaji hao kinyume cha sheria na ndipo walipomvamia na kumpiga na kusababisha kifo chake.

Hata hivyo, baada kifo hicho wakazi hao walishikwa na hasira na kuamua kujikusanya na  kulipiza kisasa kwa jamii ya wafugaji hao kwa kwa  kumuua mwenzao, Matanji Luhembe.

Luhembe alifariki baada ya kupigwa na wakazi hao waliomvamia ghafla akiwa na wenzake wakati wa harakati za kukimbia.

Luhembe alishindwa kujiokoa na kuanguka chini kutokana na tatizo la ugonjwa wa pumu na kupigwa hadi kufa.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate