Katibu
wa Kamati ya Mbio za Uhuru Marathon,Innocent Melleck (kulia)
akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza
maendeo ya Mbio hizo pamoja na Wasanii watakaotoa Burudani siku ya
Mkesha wa Uhuru itakayofanyika Desemba 8,2013 kwenye viwanja vya Leaders
Club,jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Riadha
Tanzania,Suleiman Nyambui.
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Riadha Tanzania,Suleiman Nyambui akielezea namna Mbio
hizo zitakavyoenda ikiwa ni pamoja na kuelezea njia kulingana na
makundi mbali mbali yatakayoshiriki mbio hizo.
Wasanii watamba Uhuru Marathon
ZIKIWA
zimebaki siku chache kwa ajili ya shindano la mbio ndefu za Uhuru,
Uhuru Marathon, kufanyika, wasanii watakaotoa burudani siku ya mkesha wa
uhuru wameapa kufanya kweli.
Wasanii
wanaotarajiwa kutoa burudani ni Roma Mkatoliki, Joh Makini, G Nako,
Nick wa Pili, Mrisho Mpoto, Mrisho Mpoto, TMK Wanaume, Mfalme Siboka na
kundi la Twanga Pepeta.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti, wasanii hao walisema wanashukuru kupewa heshima
kubwa kutumbuiza siku hiyo na hasa ukichukulia umuhimu wa amani, umoja
na mshikamano miongoni mwetu.
“Nitafanya
makamuzi ya kweli siku hiyo na watu wategemee mistari iliyokwenda
shule,” alisema Roma Mkatoliki, huku Mrisho Mpoto akidai ana vitu vikali
zaidi atakavyoweka hadharani siku hiyo.
Naye
Katibu wa Kamati ya Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema, homa ya
mbio hizo imepanda, hasa baada ya kujitokeza kwa wanariadha wengi wa
mataifa mbalimbali.
Melleck alisema, mbali na wengi kujitokeza bado anaamini wengi wataendelea kujiandikisha ili kufanikisha lengo la mbio hizo.
Alisema
usajili bado unaendelea kwa wale wanaotaka kushiriki ambapo fomu
zitakazotolewa kwa mshiriki wa kilomita 3 atalipa Sh 100,000 yule wa
kilomita 5 Sh 2,000 na washiriki wa kilomita 21 na 42 watalipia Sh
6,000.
No comments:
Post a Comment