Katibu
 wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa  Nape Nnauye akicheza draft na 
vijana wafanyabiashara wa soko la Sido Mwanjelwa jijini Mbeya. Nape
 yupo mjini Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za miaka 37 ya CCM 
ambazo kitaifa zitasheherekewa mkoani hapo.Katibu wa NEC alikutana na 
vijana mbali mbali ambao walifurahi sana kumuona kiongozi wao akiwa 
pamoja nao kiasi soko zima lilipuka kwa nyimbo za hamasa za CCM 
zilizoimbwa na Kapteni John Komba,Nape pia alipata fursa ya kusalimiana 
na baadhi ya madereva wa Taxi wa kituo maarufu cha Mafiati.
Katibu
 wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akila chakula cha mchana kwenye 
kibanda cha Mama Lishe anayefahamika kama Bi. Tandiwa Tewete kwenye soko
 la Sido Mwanjelwa mjini Mbeya.
 Katibu
 wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikatiza katikati ya soko la Sido
 Mwanjelwa kwenda kwenye viwanja vya mpira vya soko hilo kushuhudia 
mechi ya mpira ya wafanyabiashara wa sokoni hapo.
 Katibu
 wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiangalia mechi ya 
mpira kati ya timu ya soka ya sokoni Sido wauza Mitumba na wafungua 
Mabelo kwenye uwanja wa mpira wa sokoni Sido. 
 Katibu
 wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na 
baadhi ya viongozi wa timu za mpira sokoni Sido Mwanjelwa mjini Mbeya 
mara baada ya mpira kumalizika.
 
 
 
 
 
 
 





 
No comments:
Post a Comment