EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, January 29, 2014

Bunge lataka mgogoro Bukoba uishe

29/01/2014 | Posted by Happiness Mnale | Kitaifa | 0 comments | 184 views MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Benadetha Mshashu, ameitaka wizara husika kuhakikisha inasimamia na kuupatia ufumbuzi mgogoro wa uongozi katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba. Hatua hiyo inakuja zikiwa ni siku chache tangu aliyekuwa Meya wa manispaa hiyo, Anatory Amani, kutengua msimamo wake wa kujiuzulu baada ya taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kumtia hatiani kwa ubadhirifu wa miradi ya maendeleo aliyokuwa akiitekeleza. Akizungumza jana wakati kamati hiyo ilipokutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia, Benadetha alisema Bukoba inafuka moshi, hivyo ni vyema wizara hiyo ikasimamia sheria ili kuinusuru halmashauri ifanye kazi. Alisema kuwa halmashauri hiyo ni vyema ikanusuriwa ili itende kazi kwani baada ya ripoti ya CAG kutoka nakala zake zimegawiwa hadi mitaani. Akijibu hoja hiyo Waziri Ghasia, alisema kuwa walishakutana na kuamua kuwa meya wa manispaa hiyo ajiuzulu ama madiwani wapige kura za kumuondoa au Baraza la Madiwani livunjwe na kueleza kuwa atalifanyia kazi suala hilo. Katika hatua nyingine, Ghasia alijitetea kuwa anaitwa waziri mzigo kwa sababu Tamisemi haina meno ya kuwashughulikia watendaji kutokana na sheria za nchi zilizopo. Ghasia alisema kuwa Baraza la Madiwani wakishindwa kuwachukulia hatua watendaji, Waziri wa Tamisemi hawezi kuchukua hatua kutokana na sheria zilizopo bali wakurugenzi wanachukuliwa hatua na Waziri Mkuu. Suala la mawaziri mizigo lilijitokeza jana baada ya Mwenyekiti wa kamati hiyo Dk. Khamis Kigwangalah, kueleza kuwa mfumo wa sheria katika kuwachukulia hatua za kinidhamu wakurugenzi ni tatizo. “Sheria ya Utumishi wa Umma namba 8 ya mwaka 2002 haiko sawa, ikiwezekana ijadiliwe upya, maana kila mtu kilio ni halmashauri, mawaziri wameambiwa mizigo, kombora zimepigwa kwao, madaraka waliyopewa madiwani, wakurugenzi hawawasilikizi, wananchi wamepewa mamlaka ya kiujanja ujanja tu ya kuwashughulikia wakurugenzi. Mfumo ni tatizo. “Ziangaliwe upya sheria kama madiwani hawawezi kuwasimamia, madaraka yapunguzwe na kama mfumo huu wa sasa wa uendeshaji wa halmashauri utaendelea nyie mawaziri mtaendelea kushambuliwa tu, maana usiri wa halmashauri unasababisha urahisi wa kuiba,” alisema. Katika maazimio yake, kamati hiyo ilitaka kikao hicho kihairishwe kwa wiki mbili ili wizara hiyo iwape majibu ya kina ya hoja zilizowakilishwa zitolewe kwa maandishi ikiwemo watu wa hazina wawepo, mtindo wa ripoti uonyeshe bajeti ni kiasi gani, kilichotolewa na asilimia ionekane. Maazimio mengine ni taarifa ya kesi zilizopo mahakamani, majina ya watuhumiwa, tuhuma na hatua zilizochukuliwa kwa wakurugenzi waliodaiwa kufanya ubadhirifu sh milioni 444 katika mradi wa maboresho ya serikali za mitaa ikiwemo wizara hiyo itoe ripoti za miradi ipi imetekelezwa katika sekta ya kilimo, afya, maji na elimu. Dk. Kigwangalah ambaye ni mbunge wa Nzega alisema kuwa kwa mwaka 2014, kuwajibishana ni lazima ili kuendana na mabadiliko chanya katika kuwaletea wananchi maendeleo.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate