STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka amejifungua mtoto wa kike kwa njia
ya upasuaji mwanzoni mwa wiki hii katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili
iliyopo jijini Dar.
Akizungumza na gazeti hili, Rose Ndauka alisema anamshukuru sana
Mungu kwa kumjaalia kujifungua salama huku mwanaye huyo akiwa na afya
njema.
“Ki ukweli kabisa namshukuru sana Mungu kwa zawadi ya mtoto kwa maana
nimejifungua salama kabisa,mimi na mtoto tuko vizuri na nafurahi sana
kuingia kwenye ulimwengu mwingine kabisa wa cheo kipya cha kuitwa mama,”
alisema Rose.
Akasema hivi sasa ataweka shughuli zote pembeni kwa ajili ya kuanza
kumlea mtoto mpaka atakapofisha umri ambao anastahili kuachwa ndipo
ataendelea na shughuli zake za sanaa.
No comments:
Post a Comment