Uongozi wa Young Africans SC umepata warithi wa nafasi tatu za benchi la ufundi (Charles Boniface Mkwasa, Juma Pondamali na Dr. Suphian Juma), huku
wakiendelea na mchakato kumpata kocha mkuu ambaye atachukua nafasi ya
mholanzi Ernie Brandts aliyesitishiwa mkataba wake mwishoni mwa mwaka
2013.
Charles Boniface Mkwasa "Master" aliyekua kocha mkuu wa timu ya Ruvu
Shooting katika mzunguko wa kwanza anachukua nafasi ya aliyekua kocha
msaidizi Fred Felix "Minziro" ambaye muda wake umemalizika mwishoni mwa
mwaka 2013.
Mkwasa ambaye aliichezea Young Africans miaka ya 80's
kwa kiwango cha hali juu pia alishawahi kuwa Kocha Mkuu/Msaidizi kwa
kikosi cha Jangwani kwa vipindi tofauti jambo ambalo linamfanya aiwe
mgeni katika mitaa ya Twiga na Jangwani.
Kocha wa makipa wa timu
ya Taifa Tanzania "Taifa Stars" Juma Pondamali "Mensah" anachukua nafasi
ya aliyekua kocha wa makipa mkenya Razaki Siwa ambaye pia alistishiwa
mkataba wake mwishoni mwa mwaka 2013.
Pondamali golikipa
aliyeichezea Yanga miaka ya 80's kwa kwa kiwango cha hali ya juu hata
kufikia kuwa katika kikosi cha Tanzania kilichoshiriki mashindano ya
Mataifa Afrika nchini Nigeria mwaka 1980, sio mgeni katika timu ya Young
Africans kwani awali alishwahi kuwa kocha msaidizi kwa vipindi tofauti.
Dr
Suphian Juma anachukua nafasi ya Dr Nassoro Matuzya ambaye pia
alisitishiwa ajira yake mwishoni mwa mwaka 2013 pamoja benchi la Ufundi.
Mara
baada ya kuwapata viongozi hao watatu wa Benchi la Ufundi kikosi cha
Young Africans kesho kitaanza mazoezi jioni katika Uwanja wa Bora
Kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom pamoja
na mashindano ya Kimataifa huku kocha Mkwasa akiongoza benchi hilo la
Ufundi mpaka atakapopatikana kocha mkuu ambaye watafanya watafanya kazi
kwa pamoja.
No comments:
Post a Comment