JANGA la kusafirisha madawa ya kulevya Bongo limezidi kuwa zito
kufuatia takwimu za hivi karibuni kuonesha kwamba, idadi ya wanawake
kujihusisha na shughuli hiyo inazidi kupanda.
Akizungumza na Uwazi juzi, Kamanda wa Kudhibiti na Kuzuia Madawa ya
Kulevya Tanzania, SACP Godfrey Nzowa alisema wanawake wamekuwa ni janga
kwa kuwa wanaongoza kwa kukamatwa kutokana na kujihusisha na biashara
hiyo haramu ya ‘unga’.
NZOWA AANIKA MAMBO
Katika mahojiano maalum na
gazeti hili, Kamanda Nzowa alisema inasikitisha, inashangaza kwani kwa
kipindi kifupi cha kuanzia Desemba 11, 2013 mpaka Januari 6, 2014
watuhumiwa watano walikamatwa na unga, kati yao wanawake walikuwa wanne.
“Hata mwaka jana mpaka Juni, wengi wa watuhumiwa tuliowakamata ni
wanawake ukilinganisha na wanaume, hii ni mbinu inayotumiwa na
wasafirishaji wa mihadarati kwa kuwatumia wanawake,” alisema Nzowa.
ANAJUA KITAKACHOENDELEA
Kamanda Nzowa alikwenda
mbele zaidi kwa kusema: “Tunajua, wahusika wakiona wanawake
wanadhibitiwa sana watabadilisha na kutumia wanaume kusafirisha madawa
hayo, hii hali inatisha lakini tumeigundua.”
UWANJA WA NDEGE DAR UPENYO?
Nzowa alisema kuwa,
watuhumiwa wote hao walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar wakiwa wamepakia kete za madawa hayo
tumboni wakiyasafirisha kwenda nje ya nchi.
KUPANDA MAHAKAMANI WAKATI WOWOTE
Kamanda huyo
aliongeza kwamba wanawake watatu walikamatwa Desemba 11, mwaka jana
uwanjani hapo wakiwa na madawa tumboni wakielekea nchini China.
Aliwataja wanawake hao kwa ni, Mariam Hamad (29), mkazi wa Tabata-
Kimanga, Dar. Alikutwa na pipi zenye uzito wa gramu 670. Hadija )Abdu
(30, mkazi wa Magomeni, Dar alikutwa na kete zenye uzito wa gramu 1,227.
Wengine ni Sabrina Salum (34), mkazi wa Kiwalani, Dar. Alikutwa na
unga wenye uzito wa gramu 310 na Salama Omar (miaka haikutajwa), mkazi
wa Tabata, Dar alikutwa na madawa yenye uzito wa gramu 1,975. Alikamatwa
Januari 6, mwaka huu.
Kwa mujibu wa Kamanda Nzowa, watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani
wakati wowote kuanzia sasa mara baada ya upelelezi kukamilika.
Imeelezwa kuwa, wanawake wengi wamekuwa wakitumika kusafirisha unga
kutokana na tabia iliyokuwepo huko nyuma kwamba, walikuwa wakiaminika na
hawakuwa wakikaguliwa kwa undani walipokuwa wakipita viwanjani.
NZOWA ATAHADHARISHA
“Nawatahadharisha wale
wote, wakiwemo wanawake wenye nia au wanaofanya biashara hii haramu
kuacha kwa sababu vyombo vya dola vitawakamata,” alisema Nzowa.
WANAOGOPWA VIWANJA VYA NDEGE
Baadhi ya wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere walipohojiwa
na gazeti hili kwa sharti la kutoandikwa majina yao gazetini, walisema
wanawaogopa sana wanawake wanaosafiri siku hizi.
“Hivi sasa tunawaogopa sana wanawake wanaosafiri kwa ndege kuliko
wanaume kwa sababu wanaweza kukuingiza katika matatizo ikiwa watapenya
na madawa ya kulevya na kukamatwa hapa Dar au huko nje ya nchi,” alisema
mfanyakazi mmoja.
Alifafanua kwamba, kutokana na hilo wamekuwa wakiwapekua wanawake
kila sehemu za miili yao hata sehemu nyeti ikibidi ili kuhakikisha
hawapiti na madawa hayo uwanjani hapo.
WANAWAKE HAO WAPO MASTAA
Hivi karibuni baadhi ya
mastaa Bongo wamenaswa kwa kujihusisha na biashara hiyo. Baadhi yao
walikutwa na hatia na kuhukumiwa, wengine kesi zao zinaendelea.
Wasanii hao ni Jacqueline Patrick (alikamatwa Macau-China), Saada
Kilongo (JNIA-Dar), Agnes Gerald ‘Masogange (Afrika Kusini) na Melisa
Edward (Afrika Kusini). Pia yumo Mbongo aliyenaswa Misri aliyetajwa kwa
jina moja la Fatuma huku Sandra Khan ‘Binti Kiziwi’ akitumikia kifungo
cha miaka mitano China.
JK AKASIRIKA, AWAONYA WASANII
Akizungumza katika mkutano mmoja na wasaniiwa Rais Tanzania, Jakaya
Kikwete ‘JK’ alionesha hasira zake za wazi kwa wasanii wanaotumika
kubeba unga kwenda nje ya nchi.
JK aliwaonya wasanii wenye tabia hiyo na wale ambao wapo katika
ushawishi wa kujiingiza kwenye biashara hiyo inayopigwa vita kwa sasa
duniani kote kuacha kufanya hivyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
HABARI MBALIMBALI
‘Dk. Cheni’
‘Sharo Milionea
‘Thea’
African Women
AGNESS MASOGANGE
AK CLASSIC COSMETICS
ALI KIBA
Amanda Poshy
Ant
ANT LULU
Ashley Toto
Aunt Ezekiel
Aunty Ezekiel
AUNTY LULU
Azam Fc
Baby Madaha
BAHATI BUKUKU
Barnaba
BATULI
BBA
Beauty of the day
Belle 9
BI KIDUDE
BIBI BOMBA
Big Brother
Big Brother Africa
Bill Gates
BINTI KIZIWI
BOB JUNIOR
Bodi ya Filamu
Bongo Movie
Bongo Movies
CCM
CHADEMA
Chombezo
Christina Shusho
Chuchu hans.
Clouds Media Group
Club Bilicanas
DAR LIVE
DAVINA
Dayna Nyange
Diamond
Dida
Diva Loveness Love
Dj Ommy Crazy wa Maisha Club
DOGO JANJA
DOKI
DR.CHENI
DSTV
Dude
Dully Sykes
EBSS 2013
Elizabeth Michael
Epiq Bongo Star Search (EBSS)
ESHA BUHETI
Ester Bulaya
Feza Kessy
FIESTA 2014
Flaviana Matata
FLORA MBASHA
FLORA MVUNGI
Francis Cheka
GARDNER
GLOAL PUBLISHERS
GLOBAL TV ONLINE
H. BABA
Halima Mdee
HAMISA
Happy birthday
Hemedi
Hemedy Suleiman
HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE
Hoyce Temu
Huddah Monroe
HUSINA
IRENE PAUL
Irene Uyoya
ISABELLA
J film 4 life
Jack Chuz
JACK PATRICK
Jacob Steven ‘JB’
Jacqueline Dustan
JACQUELINE WOLPER
Jaji Khamis 'Kashi'
Jay Dee
JENNIFER KYAKA (ODAMA)
JIDE
JINI KABULA
JK
JO
Johari
Jokate Mwigelo ‘Kidot’.
JOTI
Joyce Kiria
Joyce Kiwia
JUX
K-LYNN
KADINDA
kaja
Kajala Masanja
Kapotive Star Singers
KATUNI
Kemmy
Kero Zetu
KHADIJA OMAR KOPA
KIKWETUKWETU
KILI MUSIC AWARDS
KOLETA
Lady Jay Dee
Lady Jaydee
Lake Oil
LAVEDA
Linah Sanga
Linex
Lisa Jensen
Loveness Diva
Lucy Francis Komba
Lulu
M2 The P
MABILIONEA
Madam Rita
MADELA
Magazeti
Mahusiano
Maimartha Jesse
MAINDA
MAISHA
Makala
Malkia Elizabeth
MAMTEI
MANDELA
MARIAM ISMAIL
Masanja Mkandamizaji
Mashindano ya Miss Tanzania
Matangazo
Matonya
MaxMalipo
MAYA
MELLIS EDWARD
MENINAH
MGOSI MKOLONI
Mh Halima Mdee
mic
Michezo
MILLEN HAPPINESS MAGESE
MISS CHANG'OMBE
MISS DAR CITY CENTER
Miss East Africa
MISS REDD'S IRINGA 2013
MISS TANGA 2013.
MISS TANZANIA 2014
Miss Tanzania mwaka 2011
MISS TEMEKE 2014
MISS USTAWI
MISS UTALII TANZANIA 2012/13
Miss vyuo vikuu 2013
MKALA
MREMBO HUDDAH
Mrisho Mpoto
Mrisho Ngassa
MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES.
MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013
Mtitu
muziki
Mwana FA
MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Mzee Majuto
Nancy Sumari
Nani Mtani Jembe?
NAPE
Nassoro ‘Nora’
Natasha
Nay wa Mitego
Necta
Nelly Kamwelu
NEY WA MITEGO
Nisha
NSSF;Zantel
Nyamwela
NYimbo
Nyota yako
OBAMA TANZANIA
OMMY DIMPOZ
P FUNK
PAM D
Peniel Mgilwa ‘Penny’
PETIT MAN
Profesa Jay
Q - CHILA
Q Boy
Q Chilla
QUEEN DARLEEN
RACHEL NDAUKA
RAIS KIKWETE
Rais Kikwete.
Rasimu Ya Katiba TZ
Ray
Ray C
Redd’s Miss IFM
REDD'S MISS KAGERA 2013
REDD'S MISS TZ
REDDS MISS TANZANIA 2014
Redds Miss wa Mikoa
REHEMA FABIAN
RICHIE RICHIE
Rihanna
ROSE MUHANDO
Rose Ndauka
Ruge Mutahaba.
SABASABA 2013
Saida Karoli
Saikolojia
Sajeti
SAJUKI
Sandra
SHAA
Shamsa Ford
Sheikh Ponda
Shilole
Sintah
Siwema
Skin Tricks
Snura Mushi
Spika Makinda
staa
Staa Wetu
Stella Mwangi
STYLE ZA NYWELE
Taifa Stars
Tamasha la matumaini
TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013
Tangazo
TANZANIA
TEGO
TENGENEZA WEBSITE NA BLOG
TID
Tundaman
Tupo wangapi?
TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Twanga Pepeta
USA PAGEANT 2014
VAI
Wastara
WEMA
WEMA SEPETU
Yanga
Yanga Bingwa 2013
YOUNG D
Yvonne Cherry ‘Monalisa’
Z Anton.
Zari
Zito kabwe
No comments:
Post a Comment