EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, February 25, 2014

NI AIBU ILIOJE BUNGE LA KATIBA!

NIMSHUKURU sana Mwenyezi Mungu kwa mara nyingine kwa kutuwezesha kuwa pamoja tena leo, tukijadili mambo muhimu ya taifa letu, ambalo kwa sasa lipo katika mchakato wa kupitia Rasimu ya Katiba, ambao kama utakwenda vizuri, nchi yetu itakuwa na katiba mpya wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao.

Zaidi ya Watanzania wenzetu 640 wapo katika majengo ya Bunge mjini Dodoma, wakiifanya kazi hiyo muhimu kabisa, ambayo inahitaji umakini wa hali ya juu na weledi wa kutosha, vinginevyo taifa linaweza kupata kitu ambacho kitakuwa ni hasara kwa kizazi hiki na kijacho, kwani tungetegemea suala hili angalau lilete utulivu na tofauti kwa miaka mingi ijayo.

Wajumbe hawa waliokusanyika Dodoma, ndiyo wanategemewa kutupatia katiba itakayokubaliwa na makundi yote ya wananchi, kufuatia karibu kila kada kuwa na wawakilishi wao katika bunge hili maalum la Katiba.

Tanzania kama taifa, lina changamoto nyingi sana zinazozuia maendeleo yake. Wengi wamekuwa wakisema kuwa kukwama kwetu kuendelea, kunachangiwa kwa kiasi kikubwa na matakwa ya kikatiba. Kwamba baadhi ya sheria, zinazotokana na Katiba, zinawazuia wananchi na nchi katika maeneo mengi.

Licha ya maendeleo, nchi yetu bado inahitaji amani na utulivu kwa kiwango kikubwa kuliko wakati mwingine wowote. Ni bunge hili la Katiba ndilo lenye wajibu wa kuangalia namna nzuri ya kuhakikisha maisha haya tuliyonayo, yanaboreshwa na ikiwa haina budi, kutungiwa sheria kali zaidi ilimradi tu watu waendelee kuishi bila kuogopa kitu ndani ya mipaka yao.

Kwa kutambua umuhimu wa bunge hili, asasi mbalimbali zilitakiwa kupendekeza majina ya watu wao, wanaodhani wanaweza kujenga hoja ya kulisaidia taifa, ili baadaye Rais afanye uteuzi kwa ajili ya kazi hii kubwa. Vyama vya siasa, asasi za kiraia, makundi mbalimbali ya kijamii, Bara na Visiwani, yalituma majina yao.

Kwa jinsi Bunge la Katiba (lililochagua mzee Pandu Amir Kificho, pichani, kuwa Mwenyekiti wa Muda) lilivyo na umuhimu mkubwa, kwa vyovyote, watu waliopendekezwa na makundi yao na hatimaye kuteuliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete, walitegemewa kuwa na uzalendo wa hali ya juu kwa nchi yao na wenye nia njema kabisa ya kuhakikisha Watanzania zaidi ya milioni 45 wanatengenezewa mazingira ya kuishi raha mustarehe.

Lakini katika hali inayosikitisha na kukatisha tamaa, baadhi ya wajumbe hao wameonyesha udhaifu mkubwa na kuanza kutupa hofu kama kweli dhamira ya Rais Kikwete, ya kutuletea katiba mpya, inaweza kutimia kwa kiwango kilichotarajiwa.

Inavyoonekana, wajumbe hao wamebadili nia yao ya awali ya kupigana kwa manufaa ya Watanzania, na sasa wameamua kujipigania wenyewe. Lazima niwe mkweli, nimesikitishwa sana na taarifa kwamba wenzetu hao, wanataka kupewa posho zaidi ya shilingi 300,000 ambazo hupewa kila siku tangu waliporipoti kwenye Bunge hilo maalum la Katiba kwa madai kwamba gharama za maisha zimepanda.

Huu ni usaliti mkubwa sana kwa Watanzania wanaokwenda kuwapigania. Wote tunajua maisha ya watu wetu yalivyo, leo hii kusimama na kuwaambia shilingi laki tatu kwa siku hazitoshi, ni kama kuwakebehi wananchi. Hivi maisha gani hayo wanayotaka kutuambia yamepanda? Kama wao kiwango hicho, tena cha uhakika hakiwatoshi, wanataka kutuambia mamilioni ya Watanzania wengine wanaishi vipi, ambao wengi wao wanaishi chini ya kipato cha elfu mbili kwa siku!

Kama nilivyosema mwanzo, huu ni usaliti mkubwa na aibu ya mwaka kwa wajumbe wetu. Siku zote tumekuwa tukiangushwa na watu tunaowaamini. Kama mtu anakwenda kule akifikiria kutuna kwa pochi lake, ni vipi ataweka akili zake katika hoja zinazotaka umaskini ujadiliwe na kutafutiwa mbinu za kuondolewa?
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate