EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, February 20, 2014

WABUNGE WAKATAA POSHO SH 300,000

WAKATI mjadala wa kihistoria wa kuunda Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ukiwa katika hatua ya kupata kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, baadhi ya wajumbe wameamua kuelekeza nguvu kudai posho nono.
Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa.
Wajumbe hao wanapinga posho ya sasa ya Sh 300,000 kwa siku, ambayo kwa wananchi wa kawaida inaonekana ni kubwa, lakini vielelezo vyao ni taarifa, kwamba wajumbe ambao wanatoka Baraza la Wawakilishi, wanalipwa zaidi ya hapo.

Mbali na hoja hiyo ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, ambayo sasa wajumbe ambao ni wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, wanafikiria kumbana Spika Anne Makinda, ili nao waongezwe posho kama wenzao wa Zanzibar, hoja nyingine imetajwa kuwa ni hadhi ya wabunge kwamba haifanani na Sh 300,000.

Aliyeanzisha hoja hiyo jana ni Richard Ndassa, Mbunge wa Sumve, ambaye mbali na kutaka nyongeza ya posho, alipinga utaratibu wa kusaini asubuhi na jioni kwa ajili ya posho zinazotolewa ‘rejareja’, akipendekeza waaminiwe na walipwe fedha nyingi kwa mkupuo.

Mjumbe mwingine, Suleiman Nchambi, alimwunga mkono Ndassa, lakini akahoji iweje wajumbe wa Tume ya Kurekebisha Katiba walipwe posho kubwa nao walipwe kidogo.
Mezani kwa Serikali

Kutokana na hoja hizo, Mwenyekiti wa muda wa Bunge, Pandu Ameir Kificho, alisema suala hilo linachukuliwa kwa umuhimu na watazungumza na Serikali liamuliwe baadaye.
“Kuhusu masuala ya posho, kama nilivyosema tunalichukua ili tuangalie uwezekano wa kuzungumza na Serikali, hili tutaamua hapo baadaye,” alisema Kificho.

Tume Akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge, Ndassa alisema wajumbe wa Tume walikuwa wakilipwa Sh 500,000 kwa siku huku madereva wakilipwa Sh 220,000.
“Mimi ninayehangaika kuanzia asubuhi na mimi nalipwa Sh 220,000? Mimi mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba na dereva wa Tume ni sawa?” Alihoji Ndassa.

Katika Sh 300,000 kwa siku, Sh 80,000 ndiyo posho ya kujikimu ambayo wajumbe wa Bunge la Katiba watapewa kila siku, iwe amefanya kazi au la, na Sh 220,000 ni posho ya kazi, ambayo itatolewa kwa waliofanya kazi tu.

Hadhi ya Mbunge “Mimi kwenye hizi laki tatu (Sh 300,000) zangu zote, ni pamoja na dereva wangu, simu, chakula, mafuta, lakini pia unamtaka mbunge eti lazima asaini kwanza!” Alionesha mshangao.
Bila kupendekeza kiwango cha kulipwa, Ndassa alitoa mchanganuo wa matumizi ya mbunge, akisema hoteli ya hadhi yake ni Sh 70,000 kwa usiku mmoja.
Mbali na gharama hiyo ya malazi, alisema gharama za chakula, mafuta ya gari, dereva na msaada atakaotakiwa kutoa kwa watu mbalimbali Sh 80,000 haitoshi.

“Hoja yangu ya msingi, ni kwamba Serikali ijaribu kuangalia suala hili kwa upana, tukiliacha hivi hivi linaweza kuleta tatizo,” alisema Ndassa.
Kususa

Ndassa alisema wabunge wengine ni wafanyabiashara ambao hawawezi kukubali kukaa bungeni kwa muda wote wakilipwa posho ya Sh 300,000.
Alipohojiwa anatarajia mtazamo gani kutoka kwa wananchi wanaoishi kwa kipato cha chini ya dola moja kwa siku (Sh 1,600), huku yeye akikataa Sh 300,000 kwa siku, Ndassa alisema: “Ukiweka matarajio ya jamii itasemaje, huwezi kufanya kazi. Maswali kama hayo huwezi kuyakwepa, binadamu hamwezi kulingana nyote duniani, hata vidole viko tofauti.”
Nchambi alisema kwa upande wao, wabunge hawana tatizo isipokuwa anatetea wajumbe wengine ambao hawalipwi kiinua mgongo wala mshahara.
“Mbunge anatakiwa alale kwenye hoteli ya angalau Sh 70,000. Hata wananchi wanatakiwa waelewe kwamba wabunge wamekuja kufanyia kazi Katiba ambayo ndiyo msingi wao,” alisema Nchambi.
Ubaguzi
Suala lingine lililoibuliwa na Ndassa nje ya ukumbi, ni kuhusu tofauti ya kiasi cha posho kwa alichosema wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, wameongezwa Zanzibar wakati wengine wakipokea Sh 300,000.
Bila kutaja kiasi kilichoongezwa, Ndassa alisema:“Lakini wenzetu Wazanzibari wameongezwa na Baraza la Wawakilishi, wote ni wajumbe wa Bunge hilohilo… lazima kutakuwa na mgawanyiko. Na sisi tukisema hawa wabunge wamekwenda kwao wameongezwa na sisi tumwambie Makinda atuongeze, hawa makundi maalumu watakwenda kuongezwa wapi?
“Kwa kufanya hivyo umeshaweka mgawanyiko inatakiwa tuwe kitu kimoja, kama ni Sh 20 wote tupewe Sh 20, kama ni Sh 800 wote tuwe sawa,” alisema Ndassa.
Mwandishi wa habari hizi hakufanikiwa kumpata Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Yahya Khamis Hamad kufafanua hilo kutokana na kuwa kwenye kikao.
Lakini taarifa kutoka kwa baadhi ya watendaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), zilithibitisha kwamba wawakilishi waliomba waongezwe Sh 500,000 lakini hawakupewa zote; wamepewa chini ya hapo.
“Si kweli (hawapokei Sh 420,000) lakini waliomba Sh 500,000 ila hawakupewa hizo, wamepewa chini ya hapo,” alisema mtoa habari ambaye hakusema ni kiasi walichoongezwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Utaratibu
Kwa mujibu wa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, wabunge hao wameshapewa posho ya kujikimu ya Sh 80,000 kwa siku kuanzia Februari 16 hadi 28.
Aliongeza kuwa posho maalumu ya kazi ya Sh 220,000 kwa siku, ambayo hupigiwa hesabu kutokana na ushiriki wa mjumbe kusaini mahudhurio kila siku asubuhi na jioni, itakuwa ikiingizwa kwenye akaunti za wajumbe kila baada ya wiki moja ya kazi.
CHANZO NI HABARI LEO

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate