Stori: Mwandishi Wetu, KAHAMA
MWANAFUNZI wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Majengo, Kahama mkoani Shinyanga, Said Siraji (13) anaendelea vizuri katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama alikolazwa baada ya kunusurika kifo kwa kuchinjwa shingoni na baba yake mzazi kwa madai ya kushindwa kumtibu mtoto huyo kwa matatizo yake ya afya.

Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dokta Joseph Fwoma alisema Said
anaendelea vizuri baada ya kufikishwa hospitalini hapo alfajiri ya Machi
6, mwaka huu baada kuokotwa na wasamaria wema akiwa anakimbia huku
akivuja damu shingoni.
Dokta Fwoma alisema walimfanyia upasuaji na kumshona sehemu ya
koromeo aliyochinjwa na hadi alasiri ya siku hiyo, hali yake ilikuwa
ikiendelea vizuri alipoongezewa damu.
Naye mama mzazi wa Said, Mariamu Idd (35), alisema siku moja kabla ya
tukio, baba mzazi wa mtoto huyo, Siraji Salvatory,45, (waliachana)
alikwenda kwake Majengo na kumchukua.
Mama huyo alisema asubuhi iliyofuata alishtuka sana kupigiwa simu na
nduguye mmoja akielezwa mtoto wake amechinjwa na aliyehusuka ni baba
yake mzazi.
“Kwa kweli nilishtuka sana, tena sana. Mwanangu angekufa maana baada
ya kumchinja koromeo baba yake aliamini ameshammaliza akamwacha porini
kisha yeye akakimbilia Kituo cha Polisi
Kahama kujisalimisha (hadi sasa
anashikiliwa kituoni hapo).
Mariam alisema, awali Salvatory alikuwa akimchukua Said na kwenda
naye nyumbani kwake Malunga baada ya siku kadhaa alimrudisha akidai
amechoshwa na gharama za matibabu kutokana na mtoto huyo kuwa na
matatizo ya kiafya (hakuyasema).
Jeshi la Polisi wilayani Kahakama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
No comments:
Post a Comment