EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, March 8, 2014

HOYCE TEMU ATISHIWA KUUAWA

MMOJA wa wajomba wa Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu, Jacob Temu amekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kumtishia maisha mlimbwende huyo. Tukio la kukamatwa kwa Jacob lilikuja baada ya kutishia kumuua kwa maneno Hoyce pamoja na shangazi yake ambaye ni Hilda Temu, katika mabishano ya wanaukoo juu ya sehemu ya kumzika ndugu yao, marehemu Emmanuel Nambuo Temu (33).
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu.
Hoyce aliliambia gazeti hili kuwa alitishiwa maisha kwa maneno wakati wa kikao cha wanaukoo kilichofanyika katika viwanja vya baa ya Rose Garden kujadili ni wapi pa kumzika marehemu Emmanuel, aliyefariki dunia jijini Dar Februari 16, 2014. Wakati baadhi ya wanafamilia na wosia wa marehemu wakitaka azikwe walipozikwa bibi na babu yake, Jacob alipinga hali iliyosababisha Hilda kufungua kesi katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke. Jacob alikamatwa na polisi baada ya kufunguliwa jalada yenye kumbukumbu na OB/RB/3554/2O14 KUTISHIA KUUA ambapo kesi hiyo iko katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar.


Katika kesi aliyoifungua Hilda na kusikilizwa hukumu kutolewa Jumatano iliyopita, Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Temeke, Kassim Sapi Mkwawa aliamuru mwili wa Emmanuel uzikwe katika shamba la mjomba wa marehemu Dk. Mercezederc Nambuo Temu ambaye ni kiongozi wa ukoo katika Kijiji cha Kitahie, mkoani Kilimanjaro. Awali kesi hiyo ya madai namba saba ya mwaka 2014, ilifunguliwa mahakamani hapo na Hilda Lewi Nambuo Temu, ambaye ni mama mzazi wa marehemu, akitaka mazishi ya mwanaye Emmanuel yafanyike Kijiji cha Kitahie Old Moshi mkoani Kilimanjaro lakini
Jacob alipinga. Hakimu Mkwawa wakati wa kutoa hukumu hiyo alisema:

“Baada ya kupitia maelezo ya pande zote mbili nimebaini kuwa pande zote mbili za ndugu wanachobishana si Kijiji cha Kitarara wala Kitahie bali hawataki marehemu azikwe kwenye shamba la ukoo. “Lakini kwa kuwa baba mkubwa wa marehemu Dk Mercezederc amekubali marehemu Emmanuel azikwe kando ya shamba lake lililopo Kitahie, hakuna aliyepoteza baina ya pande zote mbili, hivyo marehemu akazikwe hapo,” alisema hakimu na akasema gharama za kesi kila upande ujibebee. Kutokana na hukumu hiyo, marehemu Emmanuel anatarajiwa kuzikwa katika Kijiji cha Kitahie Old Moshi mkoani Kililimanjaro Machi 8, mwaka huu (leo), baada ya kukaa mochwari kwa siku 20.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate