EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, March 6, 2014

RAY AONESHA JEURI YA FEDHA

Na Waandishi Wetu
NYOTA wa filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ anadaiwa kumpangishia nyumba nzima mpenzi wake ambaye pia anasemekana ni mkewe mtarajiwa, Chuchu Hans, Amani lina picha kamili.
Vincent Kigosi ‘Ray’ akiwa na mkewe mtarajiwa, Chuchu Hans.
Kwa mujibu wa sosi aliye karibu na mastaa hao (jina tunalo), Ray amemwaga shilingi milioni 3,840,000 kwa ajili ya kodi ya nyumba hiyo iliyopo Mwananyamala-Msisiri B jijini Dar es Salaam.
“Wakati wanakwenda kuiona nyumba hiyo kwa mara ya kwanza, ndani ilikuwa imezeeka lakini Ray aliamua kumwaga fedha kwa ajili ya ukarabati na sasa inaonekana ni ya kifahari tena mpya, hata wewe (mwandishi) ukiingia utasema inafaa kukaliwa na staa,” alisema sosi huyo.
Nyumba aliyopangishiwa Chuchu na mumewe mtarajiwa, Ray Kigosi.
MILIONI 1,500,000 UKARABATI PEKEE
Taarifa zaidi zimejianika kwamba, staa huyo alitumia kiasi cha shilingi milioni 1,500,000 kwa ajili ya kufanyia ukarabati nyumba hiyo, kama vile kupaka rangi, kuweka dari mpya, kurekebisha milango sanjari na vitasa, kubandika marumaru na mambo mengine kibao ya kuinakshi, hali iliyowashtua watu wengi.
Nyumba hiyo inadaiwa ina vyumba vitatu vya kulala, sebuleni kubwa, jiko, bafu, choo, stoo na ua mkubwa wa kulaza magari kadhaa (kama anayo).
MASTAA WAMSHANGAA RAY
Wakati staa huyo akidaiwa kuwajibika kwa staili hiyo kwa mpenzi wake huyo, baadhi ya mastaa waliozungumza na gazeti hili walifungukia wakikikejeli kitendo hicho.

Paparazi wa GPL akiongea na hausigeli wa Chuchu.
“Hivi huyu jamaa (Ray) ana akili kweli? Au ndiyo huko kupenda? Anashindwa kuimalizia nyumba yake kule Mbezi (hakusema Mbezi ipi), anabaki kutengeneza nyumba ya watu huku akilipia kodi kubwa,”alisema staa mmoja huku akiomba chondechonde jina lake lisichorwe gazetini.
WAANDISHI MTAANI
Baada ya kuzinyaka habari hizo, waandishi wetu walijitosa mtaani kuisaka nyumba hiyo katika maeneo yaliyotajwa ya Msisiri.
CHUCHU HANS NDANI YA BAJAJ
Makadirio ya kiasi cha mita hamsini kufika kwenye nyumba hiyo, Chuchu Hans alitoka na kuingia ndani ya Bajaj yenye rangi nyekundu (namba za usajili hazikupatikana) na kuelekea kusikojulikana.
Mainda.
MAPAPARAZI WAIBAINI NYUMBA
Baada ya Chuchu kuishia, mapaparazi walibaini kuwa nyumba hiyo ndiyo ambayo Ray amejitutumua na kumpangia mrembo huyo.
Nje ya geti jeusi, waandishi walibisha hodi, akatokea msichana aliyejitambulisha ni msaidizi wa kazi za ndani katika nyumba hiyo, yaani ‘hausigeli’.
Paparazi: Tumemkuta Chuchu Hans?
Hausigeli: Hapana. Ametoka sasa hivi.
Paparazi: Amekwenda wapi?
Hausigeli: Mi sijui.
Paparazi: Hakuna mtu mwingine mkubwa mwenye kuweza kuzungumza na sisi chochote?
Hausigeli: Hakuna.
Paparazi: Haya, asante!
Hausigeli: Haya, karibuni.
Johari.
CHUCHU KWENYE SIMU YA MKONONI
Baadaye, Amani lilimpigia simu Chuchu kwa lengo la kutaka kumsikia alichonacho kuhusu nyumba hiyo, lakini simu  hiyo ilikuwa ikiita bila kupokelewa.
MSIKIE RAY
Kutokana na maadili ya taaluma ya habari, madai hayo ilikuwa lazima pia yamfikie Ray ambaye ndiye anayedaiwa kuonesha jeuri ya fedha.
Paparazi: Mambo Ray?
Ray: Poa, mzima?
Paparazi: Mi mzima tu.
Paparazi: Ee bwana, hapa ni Global Publishers, kuna ishu nataka kujua. Tumepokea habari kwamba umempangia nyumba Chuchu pale maeneo ya Mwananyamala Msisiri. Labda tuanzie hapo, ni kweli madai hayo?
 Ray: No comment (akakata simu).
Nyumbani kwa Chuchu.
JOHARI AZIDI KUKONDA
Vuguvugu la Ray na Chuchu kuwa wapenzi, kumesababisha kuharibu mfumo wa maisha ya watu waliodaiwa tangu zamani kwamba ni wapenzi wake, Blandina Chagula ‘Johari’ na Ruth Suka ‘Mainda’.
Kuzidi kupungua uzito kwa Johari kunatajwa kuwa chanzo ni Ray kummwaga yeye na kuhamishia kambi kwa mwanadada huyo. Amewahi kuulizwa kuhusu hilo lakini amekuwa mgumu wa kusema ukweli licha ya kwamba za chini ya kapeti kwa mastaa zinakiri hilo.
Kwa upande wake, Mainda alipoulizwa na Amani kuhusu anavyojisikia Ray kuwa na Chuchu alifunguka yote (yaliandikwa kwenye Gazeti la Risasi Mchanganyiko). Lakini mwisho wa maneno yake yote ni kumwachia Mungu na kwamba, ameshaamua kuishi kivyake akimwona ‘zilipendwa’ huyo kama alimpotezea muda.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate