EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, April 28, 2014

JOKATE, NATURE WATIFUANA!

Na Waandishi Wetu
PASUA jipu! Mastaa wawili wenye majina makubwa Bongo, mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Mbongo-Fleva Juma Kasim ‘Juma Nature’ wanadaiwa kuacha mshangao kwa wasanii wenzao baada ya kutifuana, Ijumaa Wikienda limeng’atwa sikio.
Mkali wa Bongo Fleva, Juma Kasim ‘Juma Nature’.
Pamoja na kwamba Nature amekuwa akizuga kutomaindi lakini habari za kushangaza zilidai kwamba mkali huyo wa Temeke amekuwa akimtuhumu mwanadada huyo kuwa amemuibia wazo lake la biashara ya ndala au kandambili.
Kabla ya madai haya mapya, Nature aliwahi kunukuliwa redioni wakati akitambulisha wimbo wake mpya wa Chuma Ulete kuwa yupo mbioni kuingiza bidhaa hiyo sokoni.
Madai ya sasa yanaeleza kwamba Nature amekuwa akilalamika kuwa Jokate ‘amekopi’ na ‘kupesti’ wazo lake la biashara.
Mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
Pia ilisemekana kwamba Nature amekuwa akimtafuta Jokate ili kuweka suala hilo sawa bila mafanikio.
“Nature amekuwa akimpigia simu Jokate lakini haipokelewi,” kilidai chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa popote hata kwa mtutu wa bastola.
Kwa mujibu wa Nature bado hajabahatika kuziona kandambili za Jokate lakini amekuwa akiambiwa na watu wake kuwa mrembo huyo kamuibia.

NATURE AFUNGUKA
Alifunguka: “Hadi sasa hivi sijabahatika kuziona hizo ndala ila nishaambiwa na watu wangu wengi tu kuwa Jokate ameniibia wazo langu.
“Mimi nasema ni wizi wa ajabu ambao sikutegemea kama Jokate angenifanyia kitu mbaya.
“Kweli sikutegemea kama ishu kama hiyo ingefanywa na mtu kama yeye (Jokate) ila hata kama ametoa mimi wazo langu liko palepale.“Nitakuja kuzitoa tu hizo kandambili zenye picha na jina langu.”
Kandambili zilizosababisha mtifuano.
BOFYA HAPA KUMSIKIA JOKATE
Baada ya kusikia upande mmoja wa Juma Nature, kama ilivyo ada kupata mzani wa habari, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Jokate na kumsomea mashitaka yake hayo ya kuiba wazo la biashara la Juma Nature.
Bila kupepesa macho wala kuchezesha masikio, Jokate alifunguka kwamba kwa upande wake anasikitishwa na mtu kama Nature kumtuhumu kwani ni kati ya watu anaowaheshimu.
Jokate alikwenda mbele zaidi na kueleza kuwa mbali na kumheshimu pia ni kaka yake.
“Wewe siyo wa kwanza kusikia tuhuma hizo kutoka kwa Nature, niliamini baada ya mimi kutoa hizo ndala, atanisapoti kwani mimi niko katika kuendeleza na kutoa ajira kwa vijana wenzangu ili kulisukuma gurudumu letu la maisha.
MASIKITIKO
“Kweli Nature amenisikitisha sana kwa kitendo chake cha kunitangazia ubaya.
“Hata hivyo, siwezi nikaacha kutoa bidhaa zangu, nitaendelea kutoa ‘so’ itabidi tu anisamehe. Kama vipi na yeye atoe za kwake,” alisema Jokate, mmiliki wa lebo ya mavazi ya Kidoti.
MASTAA WANASEMAJE KUHUSU SAKATA HILO?
Wanahabari wetu walizungumza na baadhi ya mastaa ambao walionesha kushangazwa na sakata hilo huku wakihoji kulikoni Jokate na Nature kuhitilafiana wakati kazi zao zinategemeana.
“Unajua msanii kwa msanii kutofautiana kupo tu lakini kwa Nature na Jokate unajua ni watu ambao muda wowote wanaweza kukutana kwa ajili ya kufanya kazi,” alisema mmoja wa wanamuziki wakubwa wa Bongo Fleva.
NATURE KAMGEUKA JOKATE?
Kwa mujibu wa mastaa hao, awali Nature aliposikia Jokate ana ‘aidia’ kama hiyo alinukuliwa akisema freshi tu kwani ni msanii mwenzake hivyo kipato atakachopata kitamsaidia maishani lakini kumbe inawezekana kimoyomoyo ilimuuma ndiyo maana ameendelea kumtuhumu Jokate.
KUTOKA IJUMAA WIKIENDA
Ni vyema Jokate na Nature wakakaa na kukubaliana waifanye biashara hiyo kwa pamoja kwani itawaingizia kipato kikubwa zaidi, ni kiasi cha kuona fursa na kuitumia.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate