SIKU
chache baada ya mwimbaji wa nyimbo za Injili, Rose Mhando kunusurika
kutekwa, ujumbe wa tishio la kuuawa kwa Mchungaji wa Kanisa la Huduma ya
Maombezi, Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ umesambazwa.Ujumbe huo ambao ulitumwa na mtu aliyejitambulisha kama msamaria mwema, ulisambazwa kwa watu mbalimbali mpaka kuwafikia mapaparazi wetu, unaeleza kwamba mbaya wa Rose Mhando ana mpango wa kumuua Mzee wa Upako.
Uliendelea kufafanua kwamba sababu za kuuawa kwa mtumishi huyo wa Mungu ni kwa vile ameonekana kujipendekeza kumsaidia Rose baada ya tukio lake.
Mmoja
wa waumini wa kanisa hilo, alisema kwa sasa kanisa lao lipo kwenye
maombi maalumu kwa ajili ya kumuombea kiongozi wao ili Mungu amuepushe
na hila zote za maadui.“Hawana uwezo wa kumuua mchungaji wetu maana amefunikwa na damu ya Yesu,”alisema muumini huyo.
Waandishi wetu walifunga safari mpaka kanisani kwa Mzee wa Upako na kufanikiwa kuzungumza na msaidizi wa mchungaji huyo ambaye hakutaka kutajwa gazetini, aliyekiri kusikia madai hayo, lakini akasema hawayaamini.
CHANZO:GPL

No comments:
Post a Comment