Mkurugenzi Shirika la Utangazaji
Tanzania (TBC) Clement Mshana akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni
rasmi kwajili ya kuzindua rasmi Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin
Tai Lang) uliofanyika katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Gabriel akitoa hotuba yake mbele ya
viongozi mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya
Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika siku ya jana katika Viwanja vya TBC jijini Dar es
Salaam.
Mtendaji Mkuu Kampuni ya Star Media
(T) Ltd Bw. Jack Czhou akieleza jambo wakati wa Uzinduzi wa Tamthiliya ya
Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika katika Viwanja vya
TBC jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi toka Kampuni ya
Star Media (T0 Ltd na wasanii waliotumika kuweka lugha ya Kiswahili katika
Tamthiliya ya Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) wakisikiliza kwa makini hotuba
toka kwa mgeni rasmi leo wakati wa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha
ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika katika Viwanja vya TBC jijini Dar es
Salaam.
Naibu Kati u Mkuu Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Gabriel akifurahi mara baada ya
kukata utepe ikiwa ishara ya kukamilika kwa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi
na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika katika Viwanja vya TBC
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Shirika la Utangazaji
Tanzania (TBC) Clement Mshana (kushoto) pamoja na Mshauri wa mambo ya Utamaduni
Bw. Lzu Dong (kulia) wakipeana zawadi mara baada ya Uzinduzi wa Tamthiliya ya
Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika katika Viwanja vya
TBC jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi,
Watendaji na Viongozi mbalimbali mara baada ya Uzinduzi wa Tamthiliya ya
Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika katika Viwanja vya
TBC jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE
NA BENEDICT LIWENGA.
No comments:
Post a Comment