Fatuma
Machenga (GS) mfungaji bora katika Mpira wa Pete wa mashindano ya Mei
Mosi 2014 akiwa na kikombe baada ya kutangazwa rasmi katika hafla fupi
iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuru mjini Morogoro.
Baadhi
ya wachezaji wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma (jezi za
kijani) wakishangilia kwa kutawazwa mabingwa wapya wa Mpira wa Pete Mei
Mosi 2014 kwa kuifunga timu ya Uchukuzi. Mashindano hayo yalimalizika
jana jioni katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Na. James Katubuka
Baadhi
ya wachezaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi Umma, pamoja na
mashabiki wao wakipongezana baada ya kuibuka mabingwa wapya wa Mpira wa
Pete kwa kuifunga Uchukuzi katika mashindano ya Mei Mosi 2014
yaliyomalizika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mabingwa
wapya wa Mei Mosi 2014, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
wakiwa katika mazoezi mepesi kabla ya mchezo ambao waliifunga Uchukuzi
na kunyaukua kombe la Mei Mosi 2014 iliyochezwa uwanja wa Jamhuri mjini
Morogoro.
Mchezaji
wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Sophia Komba
akijiandaa kumdhibiti mchezaji wa Uchukuzi (C) (mwenye mpira) katika
mechi ya fainali iliyochezwa katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Hekaheka
ya kuwania mpira baina ya wachezaji wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma (jezi za kijani) na Uchukuzi (jezi za bluu) katika
mechi ya fainali ya Mei Mosi 2014 iliyochezwa jana uwanja wa Jamhuri
mjini Morogoro.
Na. James Katubuka
Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma imetawazwa rasmi kuwa bingwa wa mpira wa Pete wa Mashindano ya Mei Mosi 2014.
Utumishi
imefanikiwa kuwa bingwa baada ya kuisambaratisha timu ya Wizara ya
Uchukuzi kwa ushindi wa magoli 33 dhidi ya 21. Mchezo huo wa fainali
ulifanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Katika
mchezo huo mchezaji Fatuma Machenga (GS) wa Ofisi ya Rais Utumishi
ndiye aliyekua tishio kwa kuongoza wachezaji wa timu yake kufanikisha
ushindi huo.
Mchezaji
Subira Jumanne (WA) wa Uchukuzi akizungumzia hali ya mchezo baada ya
mpira kumalizika alisema kuwa mchezo ulikuwa mgumu na wapinzani wao
walikua wamejiandaa vyema.
“Naamini
wakati wa mashindano mengine tutafanya vizuri kwa kujiandaa vyakutosha,
asiyekubali kushindwa si mshindani” Subira alisema.
Wakati
huohuo, Fatuma Machenga (GS) wa Utumishi ameibuka kuwa mfungaji bora wa
mpira wa Pete katika mashindano ya Mei Mosi 2014 kwa kufunga jumla ya
magoli 136.
“Tutahakikisha kuwa mwakani tunapambana zaidi kwa kufanya mazoezi ya kutosha ili kutetea ubingwa wetu” Machenga alisema.
Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma imenyakua kombe hilo lililokuwa
likishikiliwa na timu ya Wizara ya Ulinzi iliyokuwa bingwa katika
mashindano yaliyopita Mwaka 2013.
Mshindi wa Pili kwa mwaka 2014 ni Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mashindano hayo yalimalizika jana katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
No comments:
Post a Comment