EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, April 25, 2014

WEMA: NAJUTA KUMLIPIA KAJALA MIL 13!

Stori:Na Shakoor Jongo
KAMA kuna kitu kinakukwaza ndani ya moyo wako, siku zote ukikaa nacho kitazidi kukuumiza lakini ukiamua kumtafuta mtu ambaye umeshibana naye na kumsimulia, moja kwa moja utakuwa umeutua mzigo!
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akiwa Kajala Masanja.
Hicho ndicho amekifanya Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ kwa kuweka kweupe chanzo cha ugomvi wake na staa mwenzake, Kajala Masanja huku akijuta kumlipia mwanadada huyo zile Sh. milioni 13 za faini ili asiende jela miaka saba.
Akizungumza na Ijumaa katika exclusive interview Jumanne iliyopita, Wema ambaye pia ni staa mkubwa wa sinema za Kibongoalisema kuwa kuna mambo mazito ambayo yamesababisha yeye kuingia kwenye gogoro kubwa na Kajala.Wema au Beautiful Onyinye alisema kwamba mambo hayo ndiyo yamemsababishia maumivu ya moyo na kutokwa machozi kila wakati.
 
“Leo (anataja jina la mwandishi), ngoja nikuelezee kila kitu kinachohusiana na mimi na Kajala juu ya tofauti zetu.“Naamini baada ya kusimulia kisa na mkasa nitakuwa nimeutua huu mzigo mkubwa nilionao ndani ya moyo wangu.
“Baada ya hapo sitapenda tena kuzungumzia ishu inayonihusu mimi na Kajala,” alianza kufunguka Wema.

UZINDUZI WA KIGODORO
Katika maelezo yake, cha kwanza, Wema ni uzinduzi wa Filamu ya Kigodoro uliofanyika hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem jijini Dar ambapo yeye alisema kuwa alianza kuyaamini yale yaliyokuwa yakisemwa na watu kuhusiana na Kajala.

Wema alisema kabla ya tukio, akiwa saluni akijiandaa kwa ajili ya uzinduzi huo, ghafla Kajala alimharibia ‘mudi’. “Unajua ile Saluni ya (anataja jina la saluni) pale Kinondoni, ina sehemu mbili, juu na chini, sasa mimi nilikuwa juu na Aunt (Ezekiel) tunatengeneza nywele.
“Niliposhuka kwa ajili ya kuosha nywele, nikamuona Kajala, kwa kuwa nilikuwa sijaonana naye siku nyingi na tayari maneno yalishaanza kuwa mimi na Kajala tuna bifu, nikaona nioneshe kuwa sina bifu naye.
“Kweli nilipiga makelele ya furaha nilivyomuona K, nikawa nakimbia kwenda kumkumbatia, kiukweli niliishiwa nguvu baada ya kunikwepa na kusema nooo...Wema usinikumbatie na kuanza kutoa maneno ya dharau eti nitamchafua.

“Kusema kweli niliishiwa nguvu na kuona kama vile kizunguzungu huku aibu ikinijaa ghafla kwani pale kulikuwa na watu wengi, basi huwezi kuamini, nilishindwa kujizuia nikajikuta namtukana, sikumbakisha.
“Wakati namtukana alikuwa amekaa kwenye kiti cha kuoshwa, nikaenda nikamsukuma na kumfukuza pale kwenye kiti ili nikae nioshwe, huwezi amini hali ya hewa iliharibika ghafla kwani sikuwa na mudi tena,” alitiririka Wema.

SAFARI YA ARUSHA KATIKA SHOO YA MIRROW
Wema alisema kuwa baada ya kutofautiana pale saluni, hakuwa na kinyongo, safari ya Arusha ilipofika walikwenda kumsapoti msanii wao wa Bongo Fleva anayesimamiwa na Kampuni ya Endles Fame Production.

Wakiwa njiani, kwa mujibu wa Wema, yeye alikuwa hana fedha taslimu za kutosha zaidi ya kubeba kadi zake saba za ATM tofauti hivyo alimwambia Kajala ampe shilingi laki tatu kwa ajili ya watu kula na kunywa njiani pamoja na matumizi madogomadogo.
Alisema Kajala hakuwa na shilingi laki tatu akampa shilingi laki mbili na elfu themanini.
Aliendelea kutoa ya moyoni: “Tulipofika Arusha Kajala alimwita ndugu yake mmoja anayeitwa Doli kisha akamwambia achukue fedha alizokuwa nazo akamuwekee benki kwa sababu sikuwa na fedha na nilianza kukopa eti nilijishaua kuandaa shoo nikitegemea fedha zake.

“Wakati K anazungumza hivyo kulikuwa na watu watatu, mimi sina hili wala lile nikamuuliza mtu mmoja mbona siwaoni, wamekwenda wapi?
“Ndipo nikafungukiwa kuwa wananikimbia kisa nimemkopa K hizo laki mbili na elfu themanini, kiukweli iliniuma sana, Kanalalamikia laki mbili? Tena hakunipa bali alinikopesha?

“Nilijiuliza amesahau mimi nilitoa Sh. milioni 13 kumlipia faini asiende jela miaka saba? Nguo nikinunua nanunua sare, nywele sare, viatu sare, mapochi sare, ninachokula na kunywa mimi ndicho hichohicho.
“Siku zote wakati akiwa gerezani nguo, viatu, hereni yaani kila kitu nilikuwa ni mimi, leo laki mbili na elfu themanini, niliyomuazima ananitangazia kwa watu (anataja jina la mwandishi)?

“Iliniuma sana basi palepale, nikaenda benki nikatoa Sh. milioni mbili, nikamlipa fedha zake, nikakaa kimya nikijifanya sijui chochote kinachoendelea kwani ningefanya chochote ningeharibu shoo na isingekuwa na maana yoyote ya sisi kwenda Arusha.”
WAREJEA DAR, MAANDALIZI YA FILAMU YAKE YAANZA
Wema alisema waliporejea Dar, alimwambia Kajala kuwa kuna mtu aliyekuwa amempa stori hivyo alimuomba wafanye filamu wawili.

Alisema kwamba Kajala alikubali na kusema kuwa atachangia Sh. milioni tano katika bajeti ya filamu hiyo.Baada ya kusikia hivyo, Wema alisema alifarijika, alipokwenda kumweleza ‘bebi’ wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, naye Diamond akasema atatoa Sh. milioni tano hivyo jumla itakuwa Sh. milioni kumi ikapita bajeti iliyokuwa imepangwa ya Sh.milioni nane.
Anaendelea: “Tukiwa katika maandalizi ya mwisho tuanze ku-shoot, K alinipigia simu akaniambia hawezi ku-shoot kwani alikuwa na safari ya kwenda China labda wa-shoot vipande vyake, nikamwambia basi aende akirudi tutatengeneza nyingine.
“Baada ya kuona hivyo ndipo nikamchukua Aunt tutengeneze filamu. K alipoona nimemchukua Aunt, akanipigia simu na kuanza kuongea shiti.“Nilijiuliza mbona mwenzangu amesahau ghafla wema wangu niliomtendea au kwa kuwa tangu aanze vijisafari vyake vya kwenda China anapata
CHANZO: GPL

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate