Lady jay Dee akiwa jukwaani.
Roma mkatoliki na Baghdaddy wakifanya makamuzi.
Profesa Ludigo (Kulia) akiwa na Nikki Mbishi.
Gadner akiwa na Profesa Jay.
Shabiki akimtuza Profesa Jay.
Kutoka kushoto, Nando, Gadner na Profesa Jay.
Profesa Jay akifanya makamuzi.
Jose Mara naye alitumbuiza.
MVUA kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo
 imetibua shoo ya mkali wa muziki wa Bongo Fleva, Lady Jay Dee 
nakusababisha shoo hiyo kusogezwa mbele mpaka itakapotangazwa.
Shoo hiyo iliyopangwa kufanyika katika 
ukumbi wa Nyumbani Lounge ambapo mbali na Lady Jay Dee walikuwa 
wamealikwa wasanii wengine wakiwemo, Prof. Jay, Patricia Hillary, Roma 
mkatoliki, Baghdady na wengine kibao.
Mvua hiyo ambayo ilianza kunyesha toka 
majira ya jioni na kuzua hofu ya kuendelea kwa shoo mpaka kufikia saa 
saba za usiku mwanadada Jide alipanda jukwaani na kuomba radhi kwa 
mashabiki waliokuwa wamehudhuria ukumbini hapo kutokana na hali hiyo 
nakuwahaidi kuwa shoo hiyo itarudiwa tena ila kwa wale waliojitokeza 
watapatiwa tiketi ya shoo ijayo (Hawatalipa kiingilio tena). Baada ya 
kuomba radhi alipiga nyimbo zake kadhaa akifuatiwa na wasanii wengine.
(STORI & PICHA: Andrew Carlos na Deogratius Mongela/GPL)
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment