Nyota
wa Samba: Neymar akishangilia baada ya kuofungia Brazil bao la kwanza
katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Panama mjini Goiania
Kitu hicho! Neymar akipiga mpira wa adhabu uliozaa bao la kwanza la Brazil
Kipa wa Panama, Oscar McFarlane akidaka hews baada ya shut la mpira wa adhabu wa neymar kumpita na kiting nyavuni.
WENYEJI
wa Fainali za Kombe la Dunia, Brazil wametoa onyo- baada ya kuifumua
Panama mabao 4-0 katika mchezo wa kirafiki usiku wa kuamkia leo Uwanja
wa Serra Dourada mjini Goiania.
Neymar ameanza kuipoa ishara dunia kwamba atatisha katika fainali hizi kwa kufunga bao tamu la mpira wa adhabu dakika ya 27.
Kabla
ya mapumziko, Brazil ikapata bao la pili kupitia kwa mchezaji mwenzake
Neymar pale Barcelona, Dani Alves aliyefunga dakika ya 40.
Kipindi
cha pili kilipoanza tu, Hulk akawainua tena vitini Wabrazil kwa kufunga
bao la tatu dakika ya 46 kabla ya Willian kunaliza kazi dakika ya 73 na
kuhitimisha ushindi wa 4-0.
Kikosi
cha Brazil kilikuwa: Cesar, Dani Alves/Maicon, dk46, Luiz/Henrique,
dk70, Dante, Marcelo/Maxwell, dk46, Ramires/Hernanes, dk46, Gustavo,
Oscar/Willian, dk63, Fred/Jo, dk61, Neymar na Hulk.
Panama:
McFarlane/Calderon, dk58, Machado/Jimenez, dk56, Carroll/Rodriguez,
dk67, R Torres/Cummings, dk59, Gomez, Quintero, Cooper/Torres, dk56,
Henriquez, Munoz na Tejada/Nurse, dk46.
No comments:
Post a Comment