UGIRIKI
na Nigeria wametoka safe ya bila kufungana katika mechi yao ya
kujiandaa kwa Kombe la Dunia usiku wa jana Uwanja wa Philadelphia Union.
Kulikuwa
kuna nafasi chache za kufunga zilizotengenezwa katika mchezo huo wa
mwisho mwisho wa maandalizi kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia Juni 12.
Nafasi
nzuri zaidi waliipata Ugiriki dakika ya 83 wakati shut la Giorgios
Samaras lilipozuiliwa kutoka umbali wa mita 10 na Dimitris Salpingidis
akafuatia kupiga kichwa lakini akakosa pia.
Nigeria
ambayo ipo Kundi F pamoja na Iran, Argentina naBosnia- ilipata nafasi
nzuri nayo dakika ya 87 wakati Ogenyi Onazi alipofumua shut kutoka
umbali wa mita 25 ambako liliokolewa na kipa Stefanos Kapino.
No comments:
Post a Comment