Baadhi ya mastaa wote waliyojipatia tuzo wakiwa kwenye pozi la pamoja muda mfupi baada ya zoezi la utoaji tuzo kukamilika.
Miss Tanzania 2004, Faraja Kota (kulia), akimkabidhi tuzo ya Msanii Bora wa Filamu Anayependwa, Mzee Majuto.
Mtangazaji
wa kipindi cha Amplifier, Millard Ayo (kushoto), akipokea tuzo ya
Mtangazaji wa Redio Anayependwa Zaidi kutoka kwa Miss Tanzania 2000,
Jacqueline Ntuyabaliwe.
Meya wa Ilala, Mh.Jerry Silaa (kuli), akimkabidhi tuzo ya Mtangazaji wa Runinga wa Kike Anayependwa Zaidi, Salama Jabir.
Elizabeth Michael ‘Lulu’, akitoa neno la shukurani baada ya kutwaa Tuzo ya Muingizaji Bora wa Kike Anayependwa Zaidi.
Mbunifu
wa mavazi nchini, Mustafa Hassanali (kulia), akikabidhi tuzo ya
Mwimbaji wa Kike Anayependwa Zaidi iliyonyakuliwa na Lady Jay Dee ambapo
ilichukuliwa na mwakilishi wake, Pot Fedha.
Waandaaji
wa tuzo hizo, Nancy Sumari (kushoto) na mumewe, Lucas Neghest wakitoa
neno la shukrani muda mfupi kabla ya shughuli za utoaji tuzo kuanza.
Mdogo
wa marehemu Steven Kanumba, Seth Bosco wa kwanza kushoto na Jacqueline
Wolper wakipokea tuzo ya Filamu Inayopendwa Zaidi ya Ndoa Yangu
aliyocheza marehemu pamoja na Wolper.
Meneja
wa Kundi la Tip Top Connection, Babu Tale (kushoto), akipokea tuzo ya
Mwimbaji Bora wa Kiume kwa niaba ya Diamond ambaye yupo safarini.
Anayemkabidhi ni mtangazaji, Salama Jabir.
Mratibu wa Shindano la Bongo Star Search, Rita Poulsen (kulia), akimkabidhi tuzo ya Muongozaji Bora wa Video za muziki, Nisher.
MASTAA mbalilmbali kutoka kwenye tasnia tofautitofauti hapa nchini,
akiwemo Amri Athumani 'King Majuto', Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Millard
Ayo, usiku wa kuamkia leo wameng’ara vilivyo kwenye sherehe za utoaji
wa Tuzo za Watu ambazo zimefanyika kwa mara ya kwanza ndani ya Ukumbi wa
Serena, Posta jijini Dar es Salaam.King Majuto ameibuka kidedea baada ya kutwaa Tuzo ya Muigizaji wa Kiume Anayependwa Zaidi, huku Lulu akitwaa tuzo ya Muigizaji wa Kike Anayependwa Zaidi, Millard Ayo alikamata tuzo mbili; Mtangazaji wa Redio Anayependwa Zaidi na Kipindi cha Redio Kinachopendwa Zaidi.
Wengine walioibuka na tuzo hizo ni Nasibu Abdul ‘Diamond’, ambaye ametwaa tuzo ya Video Bora ya Muziki Inayopendwa Zaidi huku Judith Wambura 'Lady Jaydee akitwaa tuzo ya Msanii wa Muziki wa Kike Anayependwa Zaidi, Salimu Kikeke akaondoka na tuzo ya Mtangazaji wa Runinga wa Kiume Anayependwa Zaidi na Salama Jabir akachukua tuzo ya Kipindi cha Runinga Kinachopendwa Zaidi.
Aidha, Prodyuza Nisher alitwaa tuzo ya Muongozaji wa Muziki Anayependwa Zaidi na tuzo nyingine ilikuwa ya Filamu Inayopendwa Zaidi, Ndoa Yangu.
(PICHA NA MUSA MATEJA/GPL)
No comments:
Post a Comment