Wauguzi wa Hospitali ya Mwananyamala wakifurahi baada ya kukabidhiwa vifaa maalumu kwa ajili ya huduma ya uzalishaji.
Baadhi
ya manesi wakiwa na mwakilishi wa Upendo Women's Group Belgium baada ya
kukabidhi vifaa kwa ajili ya kupunguza matatizo ya kina mama wajawazito
katika Hospitali ya Mwananyamala.
Bi Begum Chunny, ambaye ni mwakilishi wa watanzania waishio Ubeligiji akitembezwa katika wodi ya mama wajawazito.
Mama huyu mjamzito alikuwa anasubiri ndugu zake waje ili anunuliwe vifaa vya kujifungulia ila Bi Begum alijitolea fedha kiasi.
Mwakilishi
wa Upendo Women's Group Belgium Bi Begum akimsalimia mama mjamzito
katika wodi ya wazazi, kushoto ni Muuguzi SP Mashauri IPDM Impatient
Department Manager.
BAADHI ya watanzania wanawake wanaoishi nchini
Ubeligiji kupitia Upendo Women’s Group Belgium wamekabidhi baadhi ya
vifaa katika wodi ya wajawazito hospitali ya Mwananyamala kwa kumtuma
mwakilishi wao ambaye yuko hapa nchini.Vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi 2,493,000/= ni pamoja na Litman Stethoscope, Ambu bag Paedreatic Bp Machine, drip stand, suction, emergency stretcher na vinginevyo.
Na Gabriel Ng’osha /GPL
No comments:
Post a Comment