Mechi hiyo ilikuwa ya marudiano ya kusaka tiketi ya kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Mabao ya Stars yamefungwa na Nadir Haroub 'Cannavaro' dakika ya 21 huku la pili likifungwa na Thomas Ulimwengu dakika ya 46. Mabao ya wenyeji Zimbabwe yamewekwa kimiani na Phiri dakika ya 10 wakati lingine likifungwa na Katsande dakika ya 55.
Kwa matokeo hayo, Stars imesonga mbele na mechi ya kwanza itakwaana na Msumbiji na ikishinda itaingia Kundi F pamoja na Zambia, Cape Verde na Niger.
No comments:
Post a Comment